Andrea Sambu na Mohamed Msenduki wafuzu madola upande wa riadha
Mohamed Msenduki |
Wanariadha Andrew
Sembu na Mohamed Msenduki wamefikia viwango vya kushiriki michezo ya
Jumuiya ya Madola vilivyowekwa na Shirikisho la riadha Tanzania (AT).
Riadha ni miongoni mwa michezo minane ya Tanzania
iliyotajwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuiwakilisha nchi kwenye
michezo ya madola itakayofanyika katikati ya mwaka huu nchini Scotland. Sambu alifikia
viwango hivyo kwenye mbio za Dazuo Marathon zilizofanyika mwishoni mwa
mwezi uliopita nchini China baada ya kutumia saa 2:14:30 kwenye marathoni
(km 42).
Msenduki ametumia saa 2:12:08 kwenye mbio nyingine za marathon
zilizofanyika nchini humo.
“Hatuwezi kuwaacha kwani wametumia muda mzuri ambao RT tuliuweka kwa
ajili ya wakimbiaji wetu wa madola,” alisema Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui.
Nyambui alisema mbali na Sambu na Msenduki pia wakimbiza upepo, Samson Ramadhan na
Osward Leverian wanajiandaa kwenda Bamaco, Mali kwenye mashindano
na wakifikia viwango watajumuishwa kwenye kikosi cha madola.
“Kamati ya ufundi ya RT iliweka muda wa kufuzu ambapo tuliamua kutumia
muda aliotumia mtu aliyekamata nafasi ya tano kwenye michezo ya madola ya
2010 nchini India,”
alisema Nyambui.
Alisema muda huo ni saa 2:12 hadi 14 kwenye marathoni muda ambao
Msenduki na Sambu wameufikia.
Akizungumzia kambi ya timu ya taifa kujiandaa na michezo hiyo, Nyambui
alisema kinachowakwamisha kuanza ni ukosefu wa fedha.
Awali kambi hiyo ilikuwa ianze Desemba Mosi mwaka jana huko Hombolo na
tayari RT iliwaita wanariadha 40 kwa ajili ya kambi hiyo licha ya
kuahirishwa mara
kadhaa.
“Programu zimekamilika japo tunakwamishwa na ukata, tukifanikiwa
kupata fedha vijana wataingia kambini japo hayo yatakuwa matunda ya
baadaye,” alisema Nyambui. Tanzania imekuwa na rekodi mbaya kwenye mashindano ya kimataifa kwa zaidi ya
miaka 10 sasa.
CHANZO: Mwananchi
NYONGEZA: Andrea Sambu alifuzu
baada ya sisi wenyewe (Siyo RT) kufanya bidii zetu kumpatia Sambu mbio nchini
China ndipo alipoweza kupata kiwango hicho.
Watanzania wafahamu hilo ‘kwamba RT
kwa sasa ni jina la mwendawazimu! Anthony
Mtaka anajenga CV aende kugombea ubunge sababu haridhiki na kazi ya DC
aliyopewa na Rais Kikwete
Naye Nyambui ‘Hajitambui’ kwa kuweka kinywani kila senti anayokumbana nayo
bila kujali masilahi ya nchi wala ya wanariadha! ‘Nyambui is a dead man walking’.
Comments
Post a Comment