Waziri Mukangara mgeni rasmi Kilimanjaro Marathon
Dr. Fenella Mukangara - Waziri |
Aggrey
Marealle, Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waratibu wa mbio hizo alisema
jana kwamba Dr. Mukangara amekubali kuwa mgeni rasmi na atahuduria sherehe ya
utoaji zawadi ambapo atatoa zawadi kwa washindi kumi wa mbio defu za kilomita
42 maarufu kama Full Marathon kwa wanaume na wanawake.
“Uwepo
wa waziri ni ishara ya uungaji mkono tukio hili na ameeleza kufurahishwa kwake
na maandalizi ya hali ya juu ya Kilimanjaro Marathon. Dk. Mukangara ameeleza mara
kadhaa kwamba serikali inaunga mkono Kilimanjaro Marathon kwa kutambua mchango
wake michezo, utalii na uchumi,” alisema Marealle.
Marealle
aliongeza kwamba baada ya sherehe ya utoaji zawadi Waziri ataungana na Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro na mpenda michezo Mhe. Leonidas Gama, wawakilishi wa
wadhamini na watu wengine mashuhuri kwenye mlo maalum wa mchana
uliodhaminiwa na Kibo Palace Hotel.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro binafsi na kupitia ofisi yake amekuwa muungaji mkono wa
Kilimanjaro Marathon na amekuwa akifurahia kukaribisha maelfu ya watu wanaokuja
Moshi kutoka mataifa mbalimbali.
John
Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema
“mbio za mwaka huu zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza
idadi ya washiriki. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42
(Kilimanjaro Premium Lager Marathon) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi
cha shilingi milioni 4 kila mmoja, shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili
na shilingi milioni 1 kwa washindi wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio
ndefu za nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi
cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa washindi wa pili na
shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.
Addison
aliongeza kuwa medali na t-shirt zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza
kumaliza mbio za kilomita 42, wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu
marathon na wanariadha 80 wa kwanza kumaliza mbio za walemavu. Washiriki
3,000 wa kwanza kumaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa
t-shirts baada ya kumaliza mbio na watapata fursa ya kujishindia zawadi
mbalimbali za kuvutia kupitia droo.
Mbio
hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa
wa Kilimanjaro na Kilimanjaro Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager, Vodacom Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel,
TPC Sugar, TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB
Tanzania, UNFPA na Kilimanjaro Water.
CHANZO: kijiwechetu.blogspot.com
Comments
Post a Comment