MUZIKI: GK atangaza ujio mpya wa East Coast Team

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Gwamaka Kaihula ‘King Crazy GK’ amewataka wapenzi wa kundi la muziki huo la East Coast Team kukaa mkao wa kula baada ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo kujipanga kurudi upya.
Baadhi ya wasanii ambao walikuwa wanaunda kundi hilo ni Ambwene Yesaya ‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, mwanadada Judith Wambura ‘Jide’ na GK.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, GK alisema, huu ni wakati wao wa kufanya kazi kama zamani kwa kutoa burudani nzuri ambazo zimekwenda shule.
“Tumeanza kuongeza nguvu katika kundi letu jipya, tunatakiwa kufanya kitu kipya katika kiwango cha juu vitu ambavyo watu hawataamini kama ni sisi,  tunatakiwa kuwa katika viwango vingine kwasababu tukiwa katika hali ilele inamaana kutakuwa hakuna maana ya kurudi upya,” alisema GK.
Alisema wameshapata studio ya kimataifa ambayo itatumika kutengenezea kazi zao, na kwamba kwasasa ataanza kutambulisha kazi yake ambayo ameshirikiana na AY na Mwana FA.


GK alishawahi kutamba na ngoma zake kama ‘Baraka au Laana’, ‘Leo’ na nyinginezo nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
CHANZO: Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga