Historia: Rais Jakaya Kikwete kufungua rasmi bunge la katiba leo

RAIS Jakaya Kikwete ana siri nzito moyoni ya kile anachotaka kuwaambia Watanzania wakati atakapolihutubia Bunge Maalumu la Katiba leo mjini Dodoma.

Hotuba hiyo inayoashiria uzinduzi rasmi wa Bunge hilo la kihistoria, inasubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wote leo ambao watalazimika kusimamisha shughuli zao kwa takribani saa tatu kumsikiliza Rais Kikwete.

Hamu ya hotuba ya Rais Kikwete inatokana na hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, aliyechambua hoja baada ya hoja kuonyesha kwamba Muungano wa Tanzania wa serikali mbili ulioachwa na waasisi, haupo tena licha ya shinikizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka kuendelea na serikali mbili.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga