KATIBA MPYA: Wafugaji wahofu Katiba kutowatambua
KUNDI la wafugaji nchini wameeleza hofu ya maisha yao kutokana na
rasimu ya pili ya Katiba kutokuwa na vipengele vinavyotambua uhalali
wao wa kuishi na shughuli wanazofanya.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Mwakilishi wa wafugaji ambaye ni
mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Makeresia Jibubu, alisema baada ya
kupitia rasimu hiyo wamebaini kuwepo na vipengele ambavyo havijaonyesha
thamani ya wafugaji nchini.
Alisema katika rasimu hiyo wafugaji wametajwa katika kipengele cha
malengo makuu na sera ya nchi na kusema ili suala la wafugaji liwe na
umhimu linapaswa liwekwe kwenye kipengele cha wajibu na haki za
binadamu, ili waweze kutambulika kisheria.
Comments
Post a Comment