KAZI KWENU WABUNGE: JK aweka wazi faida na changamoto za serikali tatu
Marais wetu wakifurahia jambo |
Katika Hotuba yake iliyofuatiliwa na wengi katika historia
ya utazamaji wa televisheni, rais Kikwete ameonyesha kutoegemea upande wowote
japo alikiri kuwa na haki ya kutoa mawazo yake.
Wengi wamefurahia uthubutu wake wa kutoegemea upande wowote
japo kwa mbali sana hisia zake ziliweza kudhihirika. Amesisitiza “Maridhiano” ndio itakayowapatia
watanzania katiba bora.
Hata hivyo makofi yaliweza kusikika kwa wingi kila alipoweza
kuelezea changamoto za muundo wa serikali tatu; kitendo kinachoashiria kwamba
wanaopenda serikali mbili wapo wa kutosha japokuwa bila maridhiano hawataweza
kupata ‘Absolute Majority” vivyo
hivyo hata wale waumini wa serikali tatu nao watahitaji ‘Political Compromise’
Mtazamo wangu:
'Katiba mpya inakuja' japo kutakuwepo na ‘Turbulence
and rough ride ahead’ Wabunge wote
waliopo Dodoma ni watanzania wenzetu,wenye masilahi sawa na sisi, wenye
uzalendo na wenye kujitambua!
Hivyo tuwaombe waanze kazi kwa kujali masilahi ya taifa la leo na lile taifa la kesho.
Hivyo tuwaombe waanze kazi kwa kujali masilahi ya taifa la leo na lile taifa la kesho.
Comments
Post a Comment