MWALIKO WA KITAIFA: Sokoine Memorial Mini Marathon inakualika Monduli Aprili 12
Gidabuday,W.F. |
Tarehe 12 Aprili 2014 Tanzania inatimiza miaka 30 tangu
kumpoteza kiongozi wake shupavu aliyefariki kwaajalimbaya ya gari Aprili 12
1984 mkoani Morogoro.
Si mwingine bali ni aliyekuwa Waziri Mkuu katika seriakali
ya awamu ya kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine aliyezaliwa 1938 wilayani
Monduli mkoani Arusha.
Ø
Tanzania itaadhimisha miaka 30 ya
kifo cha Sokoine, ni kwa kukumbuka mema yote aliyoyafanya kiasi kwamba hadi leo
anakumbukwa.
Ø
Tanzania pia mwaka huu inasherehekea
maadhimisho ‘Jubilee’ ya miaka 50 tangu nchi zetu mbili za Tanganyika na
Zanzibar ziungane.
Ø
Tanzania pia leo hii inaandaa
historia nyingine tena ‘Katiba Mpya’ huu ni mwaka wa historia ambayo
haipatikani kwingine Afrika kama si duniani.
Ø
Mimi kama mratibu wa mbio hizo ‘Race
Director’ ninapenda kuwaomba wabunge wa bunge maalum la katiba watenge siku
hiyo muhimu ya Sokoine Day kuja Monduli kusherehekea na watanzania wenzao ili
wapate ile ‘Original Spirit’ waliyokuwa nao viongozi wetu.
Ø
Bilashaka watarudi Dodoma na Baraka za
mzalendo halisi, Baraka ambazo zitawapa nguvu wabunge ili wawe na maridhiano
katika maamuzi na hatima ya katiba mpya.
Ø
Kutakuwa nambioza Half Marathon yenye
maana kamili ya “Mini Marathon” na pia kutakuwa na mbio za Kilomita 2 kwa
wanafunzi pamoja na wakubwa, katika philosophy ya michezo hakuna umri maalum!
‘Sports for All’
Ø Mwisho ninawatakia heri na safari
njema kuelekea Monduli.
“KUWA MZALENDO SAMBAZA UPENDO”
Comments
Post a Comment