SOKA LA VIJANA: Kocha Manyara aipania Arusha
KOCHA wa
Kombaini ya Mkoa wa Manyara, Mohamed Ismail, ametamba kujibua mapigo dhidi ya
Arusha katika mchezo wa maruadiano wa kusaka vipaji vya nyota wa kuboresha timu
ya taifa ‘Taifa Stars’ ambayo imeonekana kutofanya vema katika mechi zake
mbalimbali.
Mchakato huo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais
wake, Jamal Malinzi, wenye lengo la kuibua vipaji, ulianza Februari 22 katika
mikoa yote hapa nchini.
Kauli ya Ismail, imekuja baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1
kutoka kwa wenyeji wao Arusha ambao walionyesha kandanda safi na la kuvutia
katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abed jijini hapa juzi.
Ismail alisema ana imani kubwa ya kushinda katika mchezo wa
marudiano utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa Babati mkoani Manyara na kudai
kuwa, bao moja la ugenini ni faraja kubwa kwake.
“Leo tumefungwa si kusema vijana wangu si wazuri, bali wapinzani
wetu wameyatumia makosa yetu na kushinda mchezo huu, ila kusema kweli
mashindano haya ya kusaka vipaji kama Malinzi angeingia miaka kadhaa madarakani,
nina imani tungekuwa mbali kisoka,” alisema Ismail na kuongeza kuwa, nyota wa
kuunda kikosi chake aliwakusanya kutoka katika academy mbalimbali mkoani kwao
kama vile Mei, VITC, Veta, Usalama pamoja na Babati Rangers.
Naye Kocha wa Arusha, David Nyambele, aliwapongeza vijana wake
kwa kujituma hadi kuibuka na ushindi huo, huku akijivunia kuwa na nyota wengi
wazuri katika kikosi chake.
“Mimi kikosi changu kina wachezaji wazuri na wana uwezo wa hali
ya juu, pia hakuna anayezidi miaka 25, hivyo basi mimi binafsi naviona vipaji
vingi hapa nchini na si kuangalia wachezaji wa timu kubwa pekee,” alisema.
Michuano hiyo ya kusaka nyota wa kuboresha Taifa Stars
inatarajiwa kufikia tamati kesho.
CHANZO: Tanzania Daima
Comments
Post a Comment