Training Center: Tanzania inahitaji kituo kikukwa cha michezo yote
Zambia Olympic Youth Development Center |
Kilichotakiwa
na IOC ni kuhakikishiwa kwamba eneo
kubwa lisilo na utata wa kisheria linapatikana ikiwa na vithibitisho vya
kiumiliki ili hapo baadaye kusiwepo na utata (contradiction) za kisheria.
Bila aibu
wala uzalendo kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ilihakikisha kwamba kituo hicho
hakijengwi kwa sababu ya wao kuhofia masilahi yao ya upatikanaji wa tenda za
kimichezo katika center zao walizojiwekezea.
Kwa mfano: kama mtu anapata tenda ya Copa Coca-Cola ya Tsh:
Bilioni kila mwaka alafu atawezaje kupata kiasi hicho cha pesa iwapo taifa
litakuwa na center yake? Hivyo kigogo mmoja tu mwenye center yake alishawishi
kamati nzima waikatae ofa hiyo ya IOC nao kwa akili zao ndogo wakaafiki upuuzi
huo.
Hatimaye TOC ikashindwa kurudisha majibu kwa IOC ndipo IOC ikaamua kupeleka ofa hiyo Zambia na wazambia hawakuchezea nafasi hiyo na hivi sasa kuna kituo kinachoitwa Zambia Olympic Youth Development Center.
Je wizara na baraza la michezo (BMT) wamefanya juhudi gani
kuwachukulia hatua watu hao? Watu ambao
kimsingi ni ‘Wahujumu Uchumi’ maana kupindisha (Divert) masilahi ya taifa ni kuhujumu uchumi wa taifa kwani watoto
wengi wenye vipaji wangenufaika na kituo hicho bila gharama.
Comments
Post a Comment