‘Jakaya Kikwete Sports Village’ kujengwa Dom
Mfano wa ramani ya Center inayotarajiwa ya Dr. Jakaya Kikwete National Sports Village |
MAANDALIZI
ya ujenzi wa kijiji cha michezo kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Sports
Village yanaendelea vizuri, ambako tayari Ikulu, Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) na Wizara ya Michezo wametoa baraka kijengwe mjini Dodoma.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mratibu wa ujenzi wa kituo
hicho, Wilhelm Gidabuday, alisema ujenzi wa kituo hicho kikubwa na cha kwanza
nchini, tayari maandalizi yake yameshafikia pazuri na Ikulu ya Tanzania kupitia
ofisi ya Katibu wa Rais, imeshawapa baraka ya kutumia jina la Rais katika kituo
hicho.
Gidabuday alisema, wiki iliyopita walikutana na Katibu wa Rais,
ambako waliwasilisha maombi yao na kukubaliwa na kwamba, kuanzia sasa kituo
hicho ambacho ujenzi wake utasaidia kuinua vipaji vya michezo yote hapa nchini,
kitafahamika kama kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Sports
Village).
“Nidokeze tu kuwa, mipango yote inakwenda
sawa, tumeshafikisha ujumbe wetu Ikulu na imekubalika, awali tulipanga kituo
chetu tukiite John Steven Akhwari Sports Village, lakini baada ya kukaa na Mzee
Akhwari, kwa pamoja tuliridhia kituo hiki kitumike kama sehemu ya kumpa heshima
Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village,” alisema Gidabuday.
Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, hivyo kitafahamika kama Jakaya Kikwete Sports Village,” alisema Gidabuday.
Gidabuday ambaye pia anaratibu mbio za Kumbukumbu ya miaka 30 ya
kifo cha Sokoine, Sokoine Mini Marathon, pamoja na matembezi ya amani kutoka
Ujiji – Kigoma mpaka Dar es Salaam, alisema wamepanga kutumia shughuli zote
mbili kuwafahamisha wananchi kuhusu umuhimu wa ujenzi wa kituo hicho katika
maendeleo ya sekta ya michezo na utamaduni hapa nchini.
Wakati huo huo, waandaaji wa msimu wa pili wa Sokoine Mini
Marathon, zitakazofanyika Kijiji cha Monduli Juu, wametangaza rasmi sehemu
ambako fomu za ushiriki wa mbio hizo zitapatikana.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Mbio hizo,
Wilhelm Gidabuday, alisema, fomu za ushiriki wa mbio hizo kwa mwaka huu
zitapatikana wilayani Monduli, katika Kijiji cha Monduli Juu.
CHANZO: Tanzania Daima
Comments
Post a Comment