RT safari hii mkiidhulumu taifa tutafanya mapinduzi wazi wazi

Andrea Sambu Sipe
Habari za kutatanisha zinasukwa za kukata jina la Andrea Sambu Sipe asiende kuiwakilishaTanzania katika mashindano ya Jumuia ya Madola.

Sambu mwezi December mwaka jana aliweza kushiriki mashindano ya DANZHOU INTERNATIONAL MARATHON nchini China ambapo alikimbia muda wa masaa 2:14:30, muda ambao umefikia kiwango na vigezo vya kushiriki mashindano ya Commonwealth Games.

Mbali na Sambu pia kuna Musa Nduki Mohamed ambaye pia amefikia muda unaotakiwa, hivyo kwa maelezo mafupi na yanayoeleweka ni kwamba ‘Hakuna mwingine zaidi ya hao wawiwili wamefikia vigezo vya kimataifa vinavyohitajika ili kushiriki mashindano hayo ambayo yatafanyika mwezi July.

MASWALI MUHIMU: Kama kweli RT inataka Tanzania ipate medali lakini ikanuia kumwacha Sambu je watakuwa na maana gani? Haki ya mungu Ikulu tutagonga hodi iwapo Sambu ataachwa!

Sambu ni mwanariadha pekee Tanzania aliyewahi kushinda mashindano ya dunia ya mbio za nyika; Hakuna mwingine. Angalia profile yake ya ulimwengu wa riadha katika chati hapo chini.

Personal Best - Outdoor  for ANDREA SAMBU SIPE OF TANZANIA

Performance
Wind
Place
Date

5000 Metres
13:20.12

Malmö
05 AUG 1991

25 Kilometres
1:14:44

Seoul
13 MAR 2005

30 Kilometres
1:30:37

Seoul
13 MAR 2005

Marathon
2:09:52

Seoul
07 NOV 2004

World Cross Country
Champion/Winner

Antwerpen
24 MAR 1991


Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga