Glasgow: BMT na RT wametupotezea medali zetu watanzania, wamlaghai JK

Lakini pia waziri Bernard Membe amejikuta akitoa pesa za watanzania kwa wahuni waliodharau katiba ambayo ndiyo msingi wa kila kitu. Ningepata wasaa wa kumuuliza waziri Membe ningemuuliza kwamba 'Ni kwa nini hakusumbuka kupeleleza uhalali wa RT'?
Hata hivyo nampa pongezi hili 'Thanks BUT no thanks Hon. Membe' kwa kuwa ametoa pesa ambazo zilitumika kubagua wanamichezo sababu wanariadha waliokwenda kambi za nje HAWAKUSHINDANISHWA na wenzao ili kubaini nani bora atakayeweza kuiletea Tanzania medali.
Kwa maana nyingine waziri ameshiriki kubariki RT kubagua uwepo wa wanawake katika timu ya riadha ya taifa 'Ama kwa kujua ama bila kujua'
"HONGERA NYAMBUI KWA KUFANIKIWA KUMLAGHAI JK, WE MKALI UNAMDANGANYA HADI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO"
Comments
Post a Comment