Kidunda adundwa: 'Gharama ya kumdanganya mkuu wa nchi itawaumbua viongozi wa michezo'

Selemani Kidunda ambaye alikabidhiwa bendera ya Tanzania na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwa kapteni wa "Team Tanzania for Glasgow" jana amepata kipigo cha "Chap chap" kutoka kwa Kihinde Ademuyiwa wa Nigeria na kuaga mashindano moja kwa moja.

Rais Jakaya Kikwete alisema "wanamichezo wana deni la taifa hivyo taifa linasubiria medali" Hata hivyo Tanzania imeanza vibaya mashindano hayo kutokana na kinara huyo wa ngumi kupata kipigo mapema na kuaga mahindano.

Tanzania kesho itacheza karata yake muhimu wakati wanariadha Fabian Joeph Naasi na John Leonard maarufu kwa jina la Chirchir watakaposhiriki fainali za Marathon zitakazofanyika saa TATU za London sawa na aa SITA saa za Tanzania.

Balaa la timu ya Tanzania ilianza juzi ambapo mchezaji wa JUDO Ahmedi Magogo alipotolewa kabla ya kuanza mahindano kwa kutokidhi vigezo muhimu vya awali.

Balaa jingine ni majeraha ya mwanariadha Alphonce Felix kusababisha anyimwe kushiriki mita 10000 na mita 5000 na daktari wa michezo wa Glagow.

Endelea kufuatilia habari za Glasgow 2014 katika www.gidabudays.blogspot.com.


Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga