Umuhimu wa Katiba: Riadha taifa ni aibu


Ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni! Ndivyo ilivyokuwa kwenye mashindano ya taifa ya riadha yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Licha ya kukosa msisimko, aibu nyingine imelikumba Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), baada ya kukosekana kwa vijiti vya relay, namba za kukimbilia na vibendera vinavyotumika kwenye mashindano wakati wa mbio za ufunguzi hapo jana.

Gazeti hili lililokuwepo uwanjani hapo tangu mbio zinaanza lilishuhudia mmoja wa wadau wa RT akijitolea kofia yake yenye rangi nyekundu iliyotumika  kama kibendera sambamba na waandaaji kutumia karatasi nyeupe kama kibendera kingine.

Wakati wa mbio za mchujo za mita 100 mara nne, wakimbiaji walilazimika kutumia mbao zenye mfano wa vijiti vya relay kutokana na kutokuwepo kwa vijiti  halisi vya mbio hizo.

Kocha Shaban Hiki alipoulizwa juu ya vijiti hivyo alisema ni vya muda na vimetengenezwa ili viokoe jahazi.
“Vijiti halisi tumeambiwa vimeibwa hivyo vimetengenezwa hivi ‘local’,” alisema Hiki.

Huku baadhi ya wanariadha wa mbio hizo wakisikika sekunde chache kabla ya kuanza kwa mbio hizo wakidai vijiti walivyopewa kutumia ni ‘feki’.

Licha ya changamoto ya vifaa kwenye mashindano hayo,  wanariadha ambao hawajafunga Ramadhani walionekana wakirandaranda kutafuta maji ya kunywa baada ya kumaliza mbio ambayo jana yaligeuka kuwa ‘almasi’ kwenye mashindano hayo.

Kocha wa timu ya Kusini Pemba, Masoud Tawakal   alisema mashindano ya msimu huu yamekosa msisimko kulinganisha na miaka ya nyuma. “Kila kitu kiko ‘shagalabaghala’ hakuna msisimko wowote, RT inapaswa ijitathmini imekosea wapi,” alisema Tawakal. 

Akizungumzia changamoto hizo, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alisema zimechangiwa na baadhi ya watu wachache.

“Mimi sikuwepo ndiyo nimerudi, lakini fedha ya vibendera imetoka hadi sasa ‘jana saa nane’ uwanjani hazipo, maji yamenunuliwa yalipoishia haijulikani, vitu vingine sijui kwa kuwa sikuwepo,” alisema Nyambui.

CHANZO: Mwananchi

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga