AJALI BARABARANI: Rage apata ajali ya gari

MWENYEKITI wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage, jana amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya agari eneo Chigongwe, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, wakati akiingia mjini humo kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba linaloanza leo. 
 Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Tanzania Daima wakati likienda mitamboni, zilisema kuwa Rage amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma, akiwa na majeraha aliyoyapata yeye na watu wengine alioongozana nao katika gari moja.

Saa chache kabla ya ajali hiyo, Rage alizungumza na Tanzania Daima na kuuushangaa uongozi mpya wa klabu ya Simba chini ya Rais Evans Aveva kwa taarifa yake kuwa umerithishwa deni la sh. mil. 250 na kuutaka kulitolea ufafanuzi, huku yeye akiahidi kuongea na wanahabari kuzungumzia sakata hilo.

Aveva, juzi alibainisha kuwa uongozi wake unakabiliwa na changamoto nzito ya uendeshaji, baada ya kurithi deni hilo, huku wakiachiwa akaunti tupu. Alisema walichokuta ni sh. mil. 60 za usajili wa beki Shomari Kapombe kwenda Azam FC pamoja na fedha za mishahara ya Julai kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu akiwa njiani kutoka Tabora kwenda bungeni mjini Dodoma, Rage alisema amegundua upungufu mkubwa katika taarifa iliyotolewa na viongozi wa Simba katika mkutano mkuu wa wanachama juzi, kwa kudai kuachiwa deni bila kuufafanulia umma wa Watanzania ujue ukweli.
“Uongozi usiweweseke, unapouambia umma kuwa fulani kaacha deni la kiasi fulani kutokana na usajili, deni la hoteli na chakula cha wachezaji, unapaswa kufafanua usajili wa mchezaji gani anayedai pesa, hoteli gani inayotudai na kiasi gani cha pesa za chakula cha wachezaji..

Huo ndio ukweli, sio kusema deni bila kulitolea ufafanuzi,” alisema Rage. Aliutaka uongozi huo kubainisha ni kiasi gani cha pesa za usajili inazodaiwa kwa kuwataja wachezaji husika na kiasi cha kila mmoja, kuitaja hoteli inayodai na deni hilo lilitokana na Simba kutumia huduma zao kipindi gani na shilingi ngapi, lakini pia kueleza pesa za chakula cha wachezaji gani na kwa kipindi kipi.

“Niko njiani natoka Tabora kwenda bungeni Dodoma kwa ajili ya Bunge Maalum la Katiba, lakini nitakuwa na mkutano na wanahabari kule kati ya Jumanne au Jumatano, nyakati za mapumziko ya Bunge ili kuzungumzia suala hili, lakini nawasihi viongozi Simba wasikurupuke, watulie kuiondolea jamii kigagaziko kuhusu hilo,” alisema Rage.

Alienda mbali zaidi kwa kuushangaa uongozi kudai kuwa wamekuta akaunti ya klabu haina pesa, zaidi ya kuwapo sh. mil. 60 za usajili wa Kapombe na mishahara ya wachezaji ya Julai kutoka TBL, na kuhoji kama hawakukuta pesa, matumizi yao ya sasa ndani ya klabu hiyo wanafanya kutokana na pesa gani, kama sio alizoziacha yeye.

CHANZO: Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga