Bondia Mafuru akana kuugua tumbo Madola

BAADA ya Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) kusema linaendelea na uchunguzi kubaini sababu iliyofanya bondia Nasser Mafuru ashindwe kupanda ulingoni, bondia huyo anawashangaa waliosema aliugua kwani alikuwa fiti kiafya.

Mafuru hakupanda ulingoni katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ambayo yalimalizila Agosti 3, huko Glasgow, Scotland kwasababu walizodai kwamba alishikwa na tumbo la kuharisha.

Mafuru alisema kwa njia ya simu jana, kuwa alikuwa mzima na hajawahi kuumwa tangu walipofika katika mashindano hayo, na kwamba walichelewa kufika eneo ukumbini viongozi ambao aliongozana nao ndio waliotoa sababu za kuugua.

“Mimi sikuugua nilikuwa mzima, lakini tulichelewa kufika ukumbini nilikuwa nishajiandaa baada ya kufika tukakuta wanamtangaza bingwa Yule ambaye nilitakiwa kucheza naye lakini nawashangaa waliosema kwamba nilikuwa naumwa wakati tulikuwa na daktari ambaye naye hakujua kuumwa kwangu,” alisema Mafuru.

Aidha, Mafuru alisema kuna wanaosema kwamba alikosa kocha wa kumpandisha ulingoni, kwamba kwasababu walichelewa kufika hata kocha ambaye alitakiwa kumpandisha naye akawa kashaondoka.
Mafuru aliwataka Watanzania kutomfikiria kwamba alikuwa anaogopa ushindani katika mashindano hayo, si hivyo kwani alijiandaa na alikuwa na uhakika wa kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Chanzo: Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga