Okwi arejea Simba

Emmanuel Okwi /Mchezaji maarufu wa soka
HATIMAYE mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, jana amesaini kuichezea klabu yake ya zamani ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Habari zilizopatikana jana jioni, zilisema nyota huyo ambaye hatima yake ndani ya klabu ya Yanga ilikuwa gumzo kubwa, jana alitarajiwa kusaini mkakaba huo kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi kwa kipindi kingine.

Kurejea kwa Okwi Msimbazi, kunamweka katika wakati mgumu mchezaji Benard Musoti, nyota wa kimataifa wa Kenya, kwani sasa ni yeye sasa anayechungulia dirisha la kutokea, ama Pierre Kwizera.
Okwi kutua Simba, ni kama kurejea nyumbani kwani ndio klabu aliyojiunga nayo kwa mara ya kwanza nchini akitokea Uganda na kung’ara nayo, kabla ya kuihama na kujiunga Etoile du Sahel ya Tunisia na kisha Yanga.

Sheria za usajili za Ligi Kuu Tanzania Bara zinataka klabu kuwa na nyota wa kigeni wasiozidi watano na mbali ya Okwi, nyota wengine wa kimataifa katika kikosi cha Simba ni, Raphael Kiongera, Joseph Owino, Musoti, Kwizera na Amisi Tambwe.

Mapema jana kabla ya Okwi kutua Simba, benchi la timu ya Simba, lilisema bado linamuhitaji Donald Musoti na kudokeza kuwa, haliridhishwi na kiwango cha Hussein Butoyi.

Butoyi, nyota wa kimataifa wa Burundi aliyetua Simba, hivi karibuni kuziba nafasi ya Musoti aliyekuwa mbioni kutemwa, lakini akishindikana kutokana na ugumu wa mkataba wa nyota huyo. Musoti, ambaye miongoni mwa nyota Simba waliofanya vema msimu uliopita, amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Habari zilizopatikana jana kuutoka ndani ya Simba, zilisema, baadhi ya viongozi walimuhitaji Butoyi na wengine wakisapoti hatua ya benchi la ufundi kumtaka Musoti kutokana na kiwango chake.

“Benchi la ufundi, linamuhitaji Musoti aendelee kukipiga Simba, hata mimi binafsi, Musoti namuona anafaa, huyo Butoyi hamna kitu kabisa, wanaosema wanalingana uwezo sio kweli, Musoti anajua bwana,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, hadi kufikia jana asilimia kubwa ilikuwa kwa Musoti, hivyo uwezekano wa kubaki Simba, ni mkubwa kwani gharama za kuvunja mkataba wake.

CHANZO Tanzania Daima

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga