Tunasubiri aibu tena: Medali ngumu Olimpiki ya Vijana

Kwa mazingira haya ya mazoezi Tanzania itasubiri sana ushindi wa kupata medali.
Makocha wa timu za Tanzania kwenye Olimpiki ya Vijana, wamesema wana kibarua kigumu cha kuhakikisha wanarejea na medali kwenye michezo hiyo itakayoanza Jumamaosi nchini China.

Msafara wa wachezaji wanne na viongozi watatu uliondoka jana jioni na ndege ya Shirika la Qatar, na utakwenda moja kwa moja jijini Nanjing inapofanyika michezo hiyo.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, kocha wa timu ya riadha, Mwinga Mwanjala na mwenzake wa timu ya kuogelea, Ally Hamis Bamba walisema wana kibarua kigumu kwenye mashindano hayo.

“Tunakwenda kushindana, lengo letu ni kuhakikisha tunashinda, kila nchi inahitaji medali na wachezaji wetu pia wanahitaji medali, tuna kibarua kigumu cha kuhakikisha tunapambana ili kushinda,” alisema Bamba.

Wakati kocha wa riadha, Mwinga Mwanjala akisema wanakwenda kwenye mashindano hayo kama washindani, hivyo wanaamini nafasi ya kushinda wanayo.“Bahati nzuri michezo ya msimu huu tunashiriki kwa kuwa tumefikia viwango, hivyo sisi ni washindani, kushinda au kushindwa hayo ni sehemu ya matokeo, vijana wangu wako tayari kupambana,” alisema Mwanjala.

CHANZO: Mwananchi


Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga