DENIS MALLE: Mtaka na Nyambui mnasubiri nini?

Dennis Malle ni Mwl wa Mary Naali
Michezo ya 20th ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
inayofanyika Glasgow Scotland kuanzia 23July hadi 3August 2014.

Nataka kutoa maoni juu ya timu ya Tanzania iliyoenda huko Glasgow.

Kwa ujumla kuna jambo kubwa inabidi sasa Watanzania
hasa wadau wa michezo na viongozi wa michezo waamini
kuwa wanamichezo wanaopelekwa kuwakilisha nchi katika michezo ya Kimataifa wawe ni wale tu
walio katika maandalizi mazuri yaani walio mazoezini kila siku tena mazuri yaani wawe wana matokeo mazuri ya siku za karibuni kabla ya kuchaguliwa kuunda timu ya Taifa.

Kwa wenzetu walioendelea kimichezo kambi za Taifa zinatumika kuwaunganisha wachezaji kitimu tu.
Hapa kwetu ni kinyume wanaachwa wanamichezo walio sawa kwa wakati huo na kuwa chukua ambao hawako vizuri.
Hilo lilionekana wakati wa kuchagua wanariadha watakaoenda kambi nje ya nchi kwa msaada uliotolewa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernad Membe.

Chama cha Riadha RT haikufanya uteuzi mzuri
kwani kuna wanariadha walikuwa wazuri kimbio waliachwa bila sababu za msingi.
Hilo lili dhibitika wakati wa mashindano ya Taifa ya Riadha yaliyofanyika 12-13Julay 2014 Dar.

Wale waliokuwa wakiwabwaga wenzao walioenda nje walikuwa sawa tangu mwezi wa pili mwaka huu
na RT wanajua hilo.
Hakuna maandalizi ya ndani ya miezi 2 mkimbiaji kupata kiwango kipya ya kumwacha mwenzake ambaye yuko sawa na hajapumzika kufanya mazoezi.
Kauli ya baadhi ya viongozi wa RT na Wizara kusema waliopelekwa Glasgow ndiyo bora zaidi Siyo kweli hata kidogo hasa kwa upande wa riadha!

Chakushangaza utasikia waliotimiza vigezo ndio walioenda.Kumbe hawana wanalofanya kuwafanya waliosawa watimize vigezo.Kwao kigezo ya mchezaji aliye active siyo muhimu.Wakati kwa wenzetu hilo ndiyo ya kwanza!

Lingine nilishangaa kuona Katibu mkuu wa RT kwenda na timu kambini nje ya nchi kama Kocha.
Kwani kwa nafasi yake hastahili halipo kabisa kwa wenzetu kiongozi wa nafasi ile kubwa Kitaifa kujishusha kivile.Tena hapa nchini tuna Makocha wengi wa Riadha.Tulishangaa sana kuona hilo alilofany
a katibu mkuu wa RT.Hata kama ni mwalimu wa Riadha asingestahili kuchukua nafasi ya ukocha wakati bado ni kiongozi wa juu katika chama.Wakati makocha kibao wenye sifa wameachwa.

Kabla ya uteuzi wa wanariadha waliounda timu zilizopelekwa mazoezi nje ya nchi
mimi nilitoa angalizo kwa Katibu mkuu wa RT juu ya kutokuteua wachezaji wasio na viwango na juu ya waalimu wasiokuwa wakifundisha wanariadha kabla yaani kibinafsi kabla ya kuteuliwa kuandamana na timu ya Taifa.Hakulizingatia kabisa.

Kuna ubabaishaji mkubwa kwa viongozi wa juu wa RT.Ingekuwa vema katibu ajiuzulu ili abaki kuwa mwalimu nafasi ambayo naamini anaweza kwani ndiyo taaluma yake.Imeonekana utawala hawezi kabisa!Tena yeye alishakiri kabla kuwa tusitegemee medali yoyote Glasgow.
Hivyo anajua tatizo ila tangu aingie RT sasa ni miaka 8 hakuna la maana linalofanyika katika riadha Tanzania halafu anaendelea kuwa ofisini kufanya nini?

Wakati  wa mashindano ya Riadha ya Taifa mwaka huu ubabaishaji wa Viongozi wa RT ulidhirika pale michezo ilipokosa msisimko kwa wachezaji walioteuliwa na RT kuwakilisha nchi kubwagwa sana.
Pia mbio zilikuwa zinachezwa bila utaratibu maalum unaokubalika.
Mfano hapakuwa na vibendera maalum,vijiti maalum kwa ajili ya mbio za relay na Medali zilizotolewa hata hazionyeshi ni za nini kwani hazikuchapishwa.

Viongozi wa RT ya sasa kama ni wazalendo umefika wakati wa kuwajibika ama kwa kuwasikiliza wadau wanashauri nini au kujiuzulu,tuchague wengine.

Riadha inaporomoka shauri ya ubabaishaji na ubinafsi wa RT Taifa.
Kwani si wabunifu na wala hawaendi mikoani kujadiliana na Wanariadha na waalimu wao.

Inasikitisha medali ya mwisho katika michezo mikubwa ni ya tangu 2008 ambayo ilikuwa ya Shaba iliyopatikana katika michezo ya Jumuiya ya Madola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambapo msichana Mary Naali akiwa na umri wa miaka 14 tu aliiletea Taifa medali hiyo katika mbio za mita 3000 alipokuwa wa tatu na ndiyo iliyopatikana chini ya uogozi wa Katibu mkuu huyu.
Na yenyewe ilikuwa bidii binafsi ya mchezaji yule na mwalimu wake katika mazoezi yake ya kibinafsi.
Hapakuwa na motisha hata ya kauli ya kutia moyo toka RT zaidi ya Mary kuchaguliwa baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Riadha ya Taifa yaliyofanyika Singida July 2008.

RT ikibadilika au kuacha kuwa na mawazo mgando medali kibao zitakuja nchini.

Si wabunifu,angalia pamoja na kupata kiasi cha Tsh 23milioni toka kwa wadhamini wawili IPTL na UDA kwa ajili ya kufanikisha mashindano ya Riadha ya Taifa mwaka huu.Bado michezo ilifanyika chini ya kiwango.Hakuna hata certeficate kwa washindi ili kuwatia moyo vijana wale.

Natoa wito kwa wadau wa michezo ambayo michezo yao iliwakilishwa Glasgow kukosoana na kuwajibishana ikionekana uzembe wa aina yoyote.Kwani timu zote wametoka patupu.


CHANZO: Dennis Malle

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga