Hatimaye RT wakabwa mahakamani kwa madai ya Milioni 20

Suleiman Nyambui / Katibu mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania
Kampuni ya SYMAITON SAPALI & CATHY CATERING imewaburuza viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania RT kwa deni la Tsh: 20,000,000 iliyotokana na chakula cha wanariadha wakati wa mashindano ya taifa yaliyofanyika Dar Es Salaam September 2012.


Kesi hiyo (Civil Case Number 9/2014) ilifunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Temeke siku za nyuma huku viongozi wa RT wakikaidi wito wa mahakama.


Juzi (September 11, 2014) Katibu wa RT Suleiman Nyambui alihudhuria kesi hiyo baada ya mahakama kutoa amri kali ambapo angedharau amri hiyo huenda angekamatwa na kutiwa ndani.


Akihojiwa na kituo kimoja cha redio hapo jana, Nyambui alikana kesi hiyo yenye kutia doa chama cha riadha, lakini muda mfupi baadae mwanasheria wa RT Thabit Bashir alithibitisha kuwepo kwa kesi hiyo.

Hivi karibuni Suleiman Nyambui amekuwa akiandamwa kote kote hadi kutiliwa shaka katika biashara ya madawa ya kulevya! 

Akisthibitisha yeye mwenyewe katika gazeti moja kubwa la kila siku kwamba “ni kweli aliwahi kuhojiwa na kitengo maalum cha kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya”


BMT wapo wapi? Kimaadili viongozi wa RT tayari wamepoteza sifa ya kuwa viongozi kutokana na kasoro nyingi ambazo zinaendelea kujitokeza siku hadi siku huku “sikio la kufa” la Nyambui likiwa na pamba.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga