Ikangaa apigiwa debe ‘kumrithi’ Malinzi uenyekiti wa BMT
Col. Rt. Juma Ikangaa |
Habari za ndani ambazo gazeti hili ilizipata
zilieleza kuwa kati ya majina yaliyopendekezwa na Serikali, Ikangaa
anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Malinzi.
“Yalipendekezwa majina kadhaa ya watu maarufu
ambao Serikali iliona wanastahili kuongoza BMT baada ya Malinzi kumaliza
muda wake na Ikangaa ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuwa mwenyekiti,”
kilisema chanzo chetu.
Mwenyewe (Ikangaa) alipotafutwa na gazeti hili
kujua msimamo wake, hakukubali wala kukataa kutaka cheo hicho zaidi ya
kueleza hana taarifa zozote juu ya uteuzi huo.
Gazeti hili lilimtafuta, Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel
ili kujua ukweli wa habari hizo lakini ambaye hakuwa tayari
kulizungumzia suala hilo.
“Niko kwenye kikao, suala la Ikangaa kuchaguliwa
kuwa mwenyekiti wa BMT siwezi kulizungumzia labda uwatafute wenyewe BMT
waseme,” alisema Profesa Ole Gabriel kwa kifupi.
CHANZO: Mwananchi
CHANZO: Mwananchi
Comments
Post a Comment