Nyambui ataka kung’atuka RT

Katibu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui amemtaka mtu yeyote anayeweza kuongoza chama hicho ajitokeze ili yeye ang’atuke na kumwachia madaraka.

Nyambui alisema katika mahojiano kuwa yuko tayari kujiuzulu wadhifa huo ndani ya RT kama atatokea mtu ambaye anadhani akimwachia cheo hicho ataweza kuleta mafanikio katika mchezo huo.
Kigogo huyo wa RT alisema amekuwa akifanyiwa fitina na baadhi ya watu waliowahi kumshawishi kuungana nao ili wapate fursa ya kuitumia RT kufanya maovu yao, lakini walipokumbana na ‘kigingi’ chake wameanza kumfanyia fitina.
“Baadhi ya watu wananizungumzia vibaya. Lakini niko tayari kuondoka RT hata leo kama mimi ndiyo kikwazo cha mafanikio ya riadha endapo tu akitokea mtu ambaye atanithibitishia kuwa ana uwezo wa kuleta mafanikio,” alisema Nyambui.

CHANZO: Mwananchi

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga