Uzembe waitoa Tanzania michezo ya Olimpiki 2016
Tanzania haitashiriki michezo ya soka kimataifa hadi mwaka 2016
kutokana na timu yake ya vijana wa umri chini ya miaka 23
kutoshiriki michuano ya kusaka tiketi ya kushiriki Olimpiki msimu wa
2015/2016.
Kukosekana kwa timu hiyo ya U-23 kunaweza kuwa uzembe wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Katika ratiba iliyotolewa juzi na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), pazia la michuano hiyo litafunguliwa Desemba.
Katika michuano hiyo, raundi ya kwanza Rwanda
itaanza kukata utepe kwa kumenyana na Somalia wakati Kenya itacheza na
Zambia au Botswana. Kikosi hicho mara ya mwisho kilishiriki michezo
ya Afrika mwaka 2011, kikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na
kiliondolewa mapema kwenye michuano hiyo na Nigeria.
Hata hivyo, U-23 haitashiriki michuano hiyo kwa
vile Tanzania haikuthibitisha ushiriki wake huku viongozi wa juu wa TFF
wakikwepa kulizungumzia suala hilo.
Alipoulizwa juu ya suala hilo Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kwa kifupi :”Sina taarifa nipe muda nifuatilie.” Kwa upande wake, Julio akizungumzia suala hilo
alishutumu TFF kwa uzembe kwa kushindwa kufatilia wakati Tanzania mara
ya mwisho ilifanya vizuri ingawa ilitolewa hatua za mwisho.
“Kilichopo ni uzembe tu wa wahusika wameshindwa
kufuatilia.” Timu hiyo ya U23 ndiyo chimbuko la kina Shomari Kapombe,
Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na nyota wengine.
CHANZO: Mwananchi
CHANZO: Mwananchi
Comments
Post a Comment