Zitto azitaka fainali za Afrika 2017
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameishauri Serikali
isiache nafasi adimu ya kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika 2017
(Afcon) baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuliomba Shirikisho
la Soka Afrika (Caf) kuwa mwenyeji.
“Nimeona TFF wametangaza kuwa wanaomba kuandaa
Afcon 2017, watu wameipokea kwa mtazamo tofauti. Hii ni nafasi ambayo
hatutakiwi kuiacha, nchi yetu haijawahi kushiriki mashindano hayo tangu
mwaka 1980,” alisema Zitto. Alisema: “Kuna njia mbili tu za kushiriki mashindano hayo, moja ni kufuzu na nyingine ni kuandaa fainali hizo.”
“Kwa upande wetu tangu mwaka 1980 tumejaribu,
lakini tumeshindwa hivyo njia pekee ni kuandaa ili tushiriki. Hivi
mnaijua nchi inayoitwa Burkina Faso? Wao waliandaa Afcon mwaka 1998, ni nchi maskini ya
kutupwa. Tunachohitaji ni kujenga viwanja tu kwa sababu hoteli nzuri
tunazo,” alisema Zitto.
Alisema kama yeye angekuwa, angeunda kamati
maalumu ya kuomba zabuni hiyo ili kuhakikisha Tanzania inashinda kwa
kuwa njia hiyo italinufaisha taifa kwa sababu viwanja vitakarabatiwa na
pia kuandaa timu ambayo itafaa mbele ya safari.
Alisema mbali na siasa, Zitto alisema anapenda
sana soka na kwamba anaipenda sana Taifa Stars hivyo anaamini kwa
kuandaa Afcon itakuwa ni njia pekee ya kujitangaza kimataifa. “Timu ya taifa inapocheza popote nikiwa na nafasi
huwa ninakwenda na nafanya hivyo pia ili kui-support (kuiunga mkono),”
alisema Zitto.
Kauli ya Zito imekuja siku chache baada ya TFF
kujitosa kuomba kuandaa fainali hizo mwaka 2017 baada ya Libya kujitoa
kutokana na sababu za kiusalama.
Tayari TFF imeshaiandikia CAF barua kuomba uenyeji wa Afcon 2017 baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24 mwaka huu kutoa uamuzi huo.
CHANZO: Mwananchi
Tayari TFF imeshaiandikia CAF barua kuomba uenyeji wa Afcon 2017 baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24 mwaka huu kutoa uamuzi huo.
CHANZO: Mwananchi
Comments
Post a Comment