HAKI: Michezo imezingatiwa katika rasimu inayopigiwa kura?

Wajumbe wa bunge maalum la katiba linaloendelea Dodoma, bunge hilo linategemewa kufikia tamati muda hivi karibuni tena huenda lisifanikishe azma na matarajio ya watanzania.
Hapana wanamichezo nafasi hatukupewa japo majina yalipendekezwa kuingizwa katika lile kundi la 201. 

Hata hivo wanamichezo tusichukie wala kuhuzunika maana dalili zinaonyesha wazi kwamba hakuna maridhiano yatakayoleta katiba mpya kwa sasa.

Mwisho wa siku sisi “Wanamichezo” tutakuwa na thawabu sababu hatukuthubutu kujadili jambo lisilowezekana maana dalili zipo wazi.

Hata hivyo tuangalie kwa macho kwanza maana kuna msemo usemao “Anayesikiliza kwa makini ndiye anayefaidi mwishoni”. 

Ombi kwa wawakilishi wetu bungeni hivi sasa Tafadhali waheshimiwa msiwe mabubu katika kupigania haki za wanamichezo kama ambavyo mnapigia kelele ufujaji wa fedha za uma'

'Mkumbuke kwamba jasho la mshezaji ni gharama zaidi kuliko noti zinazochapishwa na Federal Reserves’

Ninyi kushindwa kutuwakilisha vyema ama kutotetea sheria # 12 ya BMT mliyoitunga ninyi wenyewe (Bunge) 1967 zitawasababisha wanamichezo kuingilia siasa ili kuwakilisha hoja za wanamichezo bungeni.

Ninasema hivyo maana wanasiasa hamchelewi kudanganyia watu mipira na ahadi za uongo ifikapo kipindi cha uchaguzi.

Lakini mnasahau kwamba viwanja vya shule za msingi na sekondari nchi nzima vimevamiwa na wanasiasa hao hao!

'Tutawauliza mambo haya mazito wakati mnatuomba kura kipindi cha kampeni; Ila mkumbuke kwamba ahadi ni deni.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga