Theresia Dismas: Mama jasiri aliyeiletea Tanzania medali ya kwanza 1965

Katika medani ya kimichezo Tanzania, historia ya kuletwa medali ya kwanza katika mshindano ya kimataifa ilitekelezwa na mwanamama Theresia Dismas
Watanzania hatukumjua na hata tukatabiri kwamba mama yetu Theresia Dismas hayupo duniani kama nilivyowahi kuandika katika blog hii. 

Ukweli ni kwamba mtanzania wa kwanza kufungua pazia la medali yupo hai na kwamba watanzania tuanze juhudi za kumtambulisha kwa viongozi wakuu wa serikali.

Nilipoandika story kuwa mwanamke ndiye aliyeleta medali wa kwanza wengi walistuka maana historia hii inayowainua wanawake ilifichwa kwa muda mrefu bila shaka kutaka kupotosha ukweli.

Jana nimepigiwa simu toka Uingereza na mtoto wa Theresia Dismas akaniambia habari yote katika blog yangu ni kweli “Isipokuwa” mama yao yupo hai na salama na anaishi Kenya!

'Mimi nilistuka na kushindwa jinsi ya kumjibu ila nilifurahi kwamba blog yangu imevumbua dhahabu iliyofichwa' na kwamba nitafanya juhudi kwa kushirikiana na wazalendo wenzangu tuweze kuandaa mwaliko (Reunion) wa mama huyo aje kutoa neno la busara, pia watanzania tumjue kwani yeye ni kioo cha jamii.

Sina shaka kabisa naamini jambo hilo ni kwa masilahi ya taifa na wengi watalifurahia, na nitafanya bidii hilo litimie maana nimefarijika sana; Iweje jina la mama yetu huyo isiwepo katika kumbukumbu za Chama Cha Riadha? "Maneno yake ya jinsi alivyofanikiwa 1965 yataleta morale kwa wasichana wa leo"

Napenda pia kuomba radhi kwa familia ya mama Theresia Dismas kwa kuandika neno 'Marehemu' hiyo haikuwa dhamira yangu bali dhamira yangu ilikuwa kuweka historia sawa.


Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga