Wanariadha walioing’arisha Tanzania Mbio za Nyika warejea
Kocha Francis John, Joseph Panga, Bazil John, Suleiman Nyambui, Alphonce Felix, Ismail Juma wakiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere. |
Wanariadha watano wa
timu ya taifa ya riadha wamewasili jana wakitoka kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia ya mbio za nyika
yaliyofanyika mjini Guiyang, China mwanzoni mwa juma hili.
Tanzania ilishika nafasi
ya sita katika nchi 51 zilizopeleka wanariadha kwenye mashindano hayo huku
Ismail Juma akitua nafasi ya tisa kati ya wanariadha 111 waliokimbia kilometa
12.
Timu hiyo iliwasili
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 10:55 jioni kwa Shirika la
Ndege la Emirates wakiongozana na Kocha wao Francis John na kupokewa na Katibu
Mkuu wa Chama cha Riadha nchini (RT) Suleiman Nyambui.
Pia mwanariadha Bazil
John alisema kuwa Tanzania isitegemee medali kama haiwekezi katika maandalizi
kwani wamejifunza mengi walipoenda kushiriki mbio hizo.
Kocha Francis John
alisema hata sasa wanariadha wamejitahidi sana kutokana na maandalizi
yaliyokuwepo.
“Inatosha kusema
wanastahili pongezi kwa kuing’arisha nchi katika medani ya kimataifa, tutajitahidi
katika michuano mingine,” alisema Kocha Francis.
Kwa upande wake Katibu nbMkuu wa RT, alisema baada ya wanariadha hao
kurudi watawaacha kwa majuma matatu kisha wamewaandalia kambi ambayo itawaleta
wanariadha 20 na makocha watatu ambao watawekwa kambini Mbulu kuanzia Aprili
28, mwaka huu kwa ajili ya mbio za majaribio za Pan African Championship zitakazofanyika nchini Uganda Mei 31.
Itakumbukwa kwamba timu
ya taifa ya Tanzania ilipeleka wanariadha watano, Fabian Nelson Sulle, John
Bazil Baynit, Joseph Panga na Ismail Juma.
Comments
Post a Comment