Gidabuday amaliza # 6 mbio za nyika Marekani

Sydney Wilhelm Gidabuday
Sydney Wilhelm Gidabuday alimaliza mbio za nyika za kilomita 10 kwa kutumia dakika 29 sekunde 39 jimbo la Missouri nchini Marekani.


Alishika nafasi ya sita kati ya wanariadha 246 ambao walifuzu kuwakilisha vyuo vyao katika mashindano ya fainali za National Collegiate Athletics Associations (NCAA)


Katika mashindano hayo Gidabuday alianguka ikiwa amebakiza kilomita tatu, alipitwa na umati mkubwa, alipoinuka alianza tena kufukuza upepo na kuwakuta wengi waliompita akafanikiwa kuishia namba sita.


Mshindi wa mbio hizo Alfred Chelanga alikimbia dakika 29 sekunde 24. Gidabuday aliiwezesha Adam State University kushika nafasi ya pili yeye akiwa mkimbiaji nambari moja wa chuo chake.


“I fell half way through, but was able to finish 6th with the time of (29:39), it socks to be beaten by those whom I know I could beat”


Gidabuday aliyasema hayo akihojiwa na Espn-Tv.

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga