Nitaanzisha matembezi ya KM 1300 kuchangisha fedha za kujenga ofisi na kambi ya kudumu ya RT.
Na Victor Machota, Arusha.
Katibu Mkuu wa chama cha Riadha Tanzania Wilhelm Gidabuday ni mmoja kati ya watanzania waliokwisha kutoa jasho, kushinda njaa na kupata maumivu, ilimradi sekta ya riadha ililetee Taifa heshima kama waasisi wa mchezo wa riadha nchini walivyojitoa hapo awali kuliwakilisha Taifa letu vyema katika mashindano ya kimataifa.
Wilhelm amekuwa mfano katika harakati za kuboresha riadha toka hata kabla hajawa kiongozi katika riadha, mfano mzuri ni pale alipoamua kutembea umbali wa kutoka Bagamoyo hadi Ujiji kuhamasisha riadha hapa nchini, huku akiungwa mkono na wazalendo wachache wenye moyo na kiu ya kuboresha riadha nchini.
Lakini pia amekua ni muanzirishi wa Sokoine Mini Marathoni ambayo hufanyika Monduli Juu kwa hayati Edward Moringe Sokoine.
Sasa leo kupitia ukurasa wake wa Facebook, Katibu Mkuu Gidabuday ameonekana kudokeza matembezi mengine makubwa. Soma hapo chini alichoandika>>>
"Sasa nalianzisha #Dude - miaka 7 iliyopita nilitembea kwa miguu toka #Bagamoyo hadi #Ujiji, njiani niliungwa mkono na wachache sana.
Muda wowote kuanzia sasa ntalianzisha tena kwa madhumuni ya kuchangisha fedha za kujenga #Ofisi na #Kambi ya kudumu ya #RT."
Gidabuday aliendelea kufunguka>>> Kutembea umbali huo ni #Maumivu, #Risky, #Sacrifice nk. Kwa ajili ya uwekezaji wa Riadha ya leo na milele #Nitatembea.
Naamini wadau wa michezo, vyombo vya habari, viongozi na watanzania wote wataniunga mkono."
Safari hii ntaanzia #Ujiji hadi Dar VIA #Bagamoyo, nasubiria ruhusa ya serikali alafu #Mapinduzi ya Riadha yaanze, ni umbali wa zaidi ya klm 1300 kwa miguu 100%."
Endelea kufuatilia dondoo kibao za KITOFAUTI duniani kupitia blog yetu ya ASILI YETU TANZANIA. Pia subscribe You Tube account yetu kupata update kibao.
Comments
Post a Comment