GIDAWAME GWAI MAGOMA: Nataka niwe mwanariadha wa kimataifa

 

Mwanariadha chipukizi (Gidawame) akikabidhiwa vifaa vya michezo na Eva Gidabuday (Mkurugunzi wa GSTF), kushoto ni Faustin Baha Sulle (mshindi wa medali ya Fedha mbio za nusu marathon za dunia Veracruz Mexico 2000) ambaye anamsimamia katika mazoezi ya mwanariadha huyo

Gidawame alizaliwa tarehe 28/12/2000 akiwa mtoto pekee kwa mama yake ambaye alifariki akiwa bado mdogo sana kiasi kwamba hakumbuki sura yake.

Baada ya mama yake kufariki akalelewa na mama wa kambo kwa sababu Baba yake alikuwa na wake tisa ikiwa ni pamoja na mama yake aliyefariki.  

“Nilipitia maisha ya mateso sana nikiwa mikononi mwa mama zangu wa Kambo, nilinyimwa haki zangu za msingi, nililazimika kuchunga ng'ombe; hata ilipofika wakati wa kuanza shule nikanyimwa kwenda shule wakati wenzangu wengine wakisoma”

Kitendo cha kunyimwa kusoma kilimumiza sana, ikafika wakati akiwa machungani anawasogeza ng’ombe karibu na shule ili aweze kuwasikia wenzake wakisoma naye apate kujifunza. Wazazi walipopata taarifa walimpa adhabu ya kuchapwa viboko na kuhakikisha hafiki katika mazingira ya shule.

Pamoja na kunyimwa kusoma, mambo mengine ambayo yalimtesa katika kukua kwake ni pamoja na kutokupata haki ya kupelekwa hospitali alipougua, muda mwingine alishinda na ng’ombe porini bila kupata msaada hadi inafikia wakati anapona bila kupata dawa wala matibabu. 

“Wakati mwingine ninapozidiwa sana nililala porini hadi siku iliyofuata nipate kujongea nyumbani”

Mateso yalipozidi sana kwa kukata tamaa aliamua kunywa sumu ya kuogeshea mifugo, bahati nzuri haikuweza kuleta madhara makubwa kwani alipona baada ya kuokolewa na msamaria mwema.


Alitembezwa kilomita nyingi sana kwenda nyumba moja hadi nyingine akiwa anachukuliwa kama kijana wa kazi badala ya mtoto, alipochelewa njiani kwa mwendo mrefu aliishia kuchapwa sana.

Wakati akiendelea kupitia magumu haya hadi kufikia umri wa kujitambua ndipo alipogundua kuwa ana vipaji vingi ndani mwake, akaanza kupenda kucheza, mchezo wa kwanza kuupenda ni kurusha mkuki na riadha.

Akaamua kwamba kwa vile ndoto yake kubwa ni kupata elimu kupitia kucheza anaweza kupata nafasi ya kujisomesha mwenyewe akiweza kutoka katika mazingira haya yanayomgandamiza.

Kwa juhudi zake binafsi Gidawame tayari alishapata medali ya Shaba 2019 na ya Fedha 2020 katika mashindano ya Taifa ya Riadha kurusha mkuki (Javelin). Pia amejua kusoma na ana uwezo mkubwa sana wa kumudu mitandao ya kijamii ambapo anaendelea kujifunza.

Baada ya kukutana na makocha wa Arusha Gidawame tayari amepata vifaa vya mazoezi na ameanza mazoezi rasmi ambapo ameshauriwa atakuwa mzuri kwa mbio za mita 1500 hadi mita 10000 ambapo makocha hao wataendelea kumfundisha kwa kujitolea hadi afikie ndoto zake. 

Supported by;

 https://oregesafariandtours.com/

 

 

 

 

Comments

Popular

GIDABUDAY KUHAMASISHA UJENZI WA KIJIJI CHA MICHEZO TANZANIA LENYE JINA YA MWANARIADHA MKONGWE BW.JOHN STEPHEN AKHWARI

Rio Olympics: Brazil win men's volleyball gold, GB's Joyce takes boxing silver – as it happened

Olympics 2016: Usain Bolt completes sprint double, Jade Jones retains taekwondo title

Rio Olympics: Swimmer Lochte apologises for 'robbery' saga