Nitaanzisha matembezi ya KM 1300 kuchangisha fedha za kujenga ofisi na kambi ya kudumu ya RT.
Na Victor Machota, Arusha. Katibu Mkuu wa chama cha Riadha Tanzania Wilhelm Gidabuday ni mmoja kati ya watanzania waliokwisha kutoa jasho, kushinda njaa na kupata maumivu, ilimradi sekta ya riadha ililetee Taifa heshima kama waasisi wa mchezo wa riadha nchini walivyojitoa hapo awali kuliwakilisha Taifa letu vyema katika mashindano ya kimataifa. Wilhelm amekuwa mfano katika harakati za kuboresha riadha toka hata kabla hajawa kiongozi katika riadha, mfano mzuri ni pale alipoamua kutembea umbali wa kutoka Bagamoyo hadi Ujiji kuhamasisha riadha hapa nchini, huku akiungwa mkono na wazalendo wachache wenye moyo na kiu ya kuboresha riadha nchini. Lakini pia amekua ni muanzirishi wa Sokoine Mini Marathoni ambayo hufanyika Monduli Juu kwa hayati Edward Moringe Sokoine. Sasa leo kupitia ukurasa wake wa Facebook, Katibu Mkuu Gidabuday ameonekana kudokeza matembezi mengine makubwa. Soma hapo chini alichoandika>>> "Sasa nalianzisha #Dude - miaka 7 iliyopita nilitembea kw