Mkutano wa Katiba RT waota mbawa
Suleiman Nyambui/Katibu RT MKUTANO mkuu wa kupitisha rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), uliokuwa ufanyike mjini Morogoro Novemba 30 umepigwa kalenda. Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui , alisema mkutano huo umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena baada ya kuingiliana na sherehe za ujio wa Kombe la Dunia litakalowasili nchini Novemba 29. Alisema tayari ameanza kuwatumia taarifa wajumbe mbalimbali wa mkutano huo kupitia njia ya barua na mtandao ili kuhakikisha taarifa hizo zinawafikia kwa wakati na kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwao. “Viongozi wote watakuwepo katika sherehe hizo, hivyo kamati ya utendaji imeona isogeze mbele mkutano ili kuwapa nafasi wajumbe wetu kulishuhudia kombe hilo, na ninaamini taarifa zitamfikia kila mmoja na hakutakuwa na tatizo lolote,” alisema Nyambui. Kutokana na hali hiyo, aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuwa wavumilivu na kujiandaa kwa ajili ya mku...