RIADHA: Ikangaa awalipua wanariadha
K anali Mstaafu Juma Ikangaa Mwanariadha wa zamani, Juma Ikangaa, amesema wanariadha wengi wa Tanzania wanaponzwa na kutokuwa wakweli, huku akibainisha kuwa kutokuwapo kwa mkimbiaji wa mbio ndefu, Samson Ramadhan kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola msimu huu ni pigo kwa Taifa. Kauli ya Ikangaa imekuja siku chache baada bingwa huyo wa marathoni wa michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2006, kuondolewa kwenye kikosi cha Tanzania kitakachoshiriki michezo hiyo msimu huu. Wiki iliyopita, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid, alisema Ramadhan ambaye yuko kambini nchini China kujiandaa na michezo hiyo hataweza kushiriki kwa kuwa ni majeruhi na kama kutakuwa na uwezekano atarejea nchini kabla ya kambi hiyo kumalizika. Akizungumza na gazeti hili jana, Ikangaa alisema kuondolewa kwa Ramadhan kwenye kikosi hicho ni pigo. “Kutokuwa na mwanariadha huyo ni pigo kwa taifa, hata hivyo walifanya makosa, wasingemjumuisha kwenye wanariadha waliokwenda nje kwani awali nilisikia ni...