JITIHADA BINAFSI: HOLILI YOUTH ATHLETIC CLUB (HYAC) ILIANZA KWA JUHUDI ZA MTU BINAFSI KAMA HIVI
Viongozi wa HYAC L-R (Nelson Mrashani,Domician Genand na Timoth Kamili Holili Youth Athletic Club ni moja ya vilabu vya riadha vilivyoanzishwa hapa nchini, club hii ipo Holili wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro. Club hii ilianzishwa na mdau mkubwa wa mchezo wa riadha ambaye ni mkurugenzi kwa sasa DOMICIAN RWEZAURA GENANDI mnamo 2010 na kusajiliwa rasmi 2011 kwa namba ya usajili NSC9833 na kuanza shughuli za kuendeleza mchezo wa riadha mwaka moja baadaye. Clu hii ilianza na wachezaji 6 tu lengo lake likiwa kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana katika mchezo wa riadha hapa nchini, hadi sasa club ina jumla ya wanariadha 15 wakiwemo wazoefu wachache na chipukizi ambao kwa pamoja wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano mbalimbali walioshiriki ndani na nje ya nchi. Malengo makubwa ya club hii ni kukuza na kuendeleza mchezo wa riadha kwa kuwalea wanariadha chipukizi ili waje kufanya vizuri baadaye, kuwepo kwa wanariadha wazoevu katika club kumewapa ham