Posts

Rais Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa mikoa mitano na kuwahamisha makatibu tawala wengine na wakurugenzi wa majiji

Image
Sipora J. Liana Makatibu tawala wapya ni ndugu Wamoja A.Dickolangwa anayeenda mkowa wa Iringa ambako alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa.  Ndugu Abdallah D.Chikota anayeenda Lindi kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Newala, ndugu Symthies E.Pangisa a nayeenda mkoa wa Rukwa kabla alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara, ndugu Alfred C.Luanda aliyeteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa Mtwara kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora.  Pia dugu Jackson L.Saitabau anakwenda mkoa wa Njombe kabla alikuwa katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Arusha. Waliohamishwa ni pamoja na Beatha Swai kutoka katibu tawala mkoa wa Pwani kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI, pia yupo ndugu Sipora J.Liana kutoka mkurugenzi wa jiji la Arusha kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI na ndugu Benedict ole Kuyan kutoka katibu tawala mkoa wa Tanga kwenda katibu tawala mkoa wa Mara. Wengine ni ndugu Salum M.Chima kutoka katibu tawala Rukwa kwenda Tanga na Ndug

Kikwete awatia hofu watarajiwa wa uwaziri huku wengine wakifunga novena kumomba mungu wasipigwe chini

Image
James Lembeli "The Man Ikulu yageuka mbingu ya pili kwa kile kinachodaiwa sala zote lazima iombe huruma za mungu angalau rais awateue. Hadi hii leo hii ni takriban mwezi mzima umepita tangu kutenguliwa kwa mawaziri wanne baada ya kuguswa moja kwa moja na kashfa ya Operation Tokomeza Ujangili. Mawaziri waliolazimika kujiuzulu ni pamoja na Emmanuel Nchimbi - Mambo ya ndani, Shamsi Vuai Nahodha - Ulinzi, David Mathayo – Mifugo na Khamis Kagasheki – Maliasili na Utalii.  Pigo lingine kwa baraza la mawaziri ni pale Tanzania ilipompoteza aliyekuwa waziri wa fedha Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia masaa machache kabla ya mwaka 2014 kuanza. “Rais Kikwete kipindi hiki ana kazi nzito ya kufanya; siyo kuteua mawaziri pekee! Kumbuka wabunge wa bunge maalum la katiba nao wapo katika process ya kuteuliwa” Chanzo cha kuaminika kilisema. “Anaweza kuamua kuendelea na uteuzi wa wabunge wa katiba ndipo atangaze zote kwa pamoja” mtoa habari alisema hayo kwa kifupi.  A

OFISI ZA BUNGENI: MHE. MIZENGO PINDA AKAGUA MAENDELEO YA UKARABATI WA JENGO LA BUNGE LA TANZANIA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa ameketi wakati akikagua marekebisho yanayofanyika katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18, 2013 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. (Picha ya Juu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua kazi ya uwekaji viti vipya katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Januari 18,2014 ikiwa ni maandalizi ya Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwezi ujao. (Picha ya Chini)

Wabunge watapeliwa: Wamwaga fedha kusaka uwaziri, Ikulu yatoa kauli nzito kuwaonya, JK kutangaza Mawaziri wapya leo

Image
IKULU imewaonya wabunge wenye uchu wa kuwa mawaziri na mawaziri wanaotaka kubaki kwenye madaraka hayo wasikubali kurubuniwa na matapeli wanaojifanya maofisa Usalama wa Taifa ambao wanawataka kutoa fedha ili wasaidiwe kupata uwaziri. Onyo hilo limetolewa wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kutangaza Baraza jipya la Mawaziri leo baada ya kuwang’oa mawaziri wanne na mmoja kufariki dunia. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema hakuna sababu za wabunge kukubali kutapeliwa kwa ajili ya kusaka uwaziri kwani mwenye mamlaka ya uteuzi ni Rais Kikwete na hakuna mwenye uwezo wa kuingilia uteuzi wake au kumshawishi afanye upendeleo. Mbali ya kuwaonya wabunge na mawaziri hao, Balozi Sefue pia aliwaonya matapeli wanaotumia jina la Ofisi  ya Rais Ikulu kujifanya maofisa wa Idara ya Usalama kuwarubuni watoe fedha ili wawasaidie kuingia kwenye Baraza jipya la Mawaziri. Kwa mujibu wa Balozi Sefue, wabunge wanapaswa kuwapuuza matapeli