Posts

Rais Kikwete afungua mkutano wa baraza la vyama vya siasa

Image
Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wakati wa ufunguzi wa   mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Viongozi walitanguliza neno la mungu kabla ya mkutano kuanza ikiwa ni ishara ya amani miongoni mwao wote licha ya tofauti zao za kisiasa.

WINTER OLYMPICS: Three days to go for Sochi Winter Olympics to start

Image
The teams from all over the world will be able to leave their wishes of peace on the Olympic Truce Wall that just opened in Sochi as part of the long-term Olympic tradition.  One of the Volunteers developed the design of the Wall, which is made of five panels representing the Olympic rings. The height of the Wall blocks alternates between 1924 and 2014 mm, the very first and the current year of the Winter Olympics.

Kikwete: Wajumbe Bunge la Katiba kutangazwa leo, kesho

Image
Rais Jakaya Kikwete amesema uteuzi wa majina 201 ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba umekamilika na kati ya leo na kesho, atayatangaza pamoja na tarehe ya kuanza kwa Bunge hilo. Bunge la Katiba litakalokuwa na wajumbe 640, litakutana kwa siku 90 kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Desemba 30, mwaka jana. “Bunge la Katiba litakutana katika wiki ya tatu ya mwezi huu. Mambo yanayosubiriwa ni mawili tu, uteuzi wa wajumbe 201 na siku ya kuanza kwa Bunge hili. Mambo haya yote ninayesubiriwa kuyakamilisha ni mimi tu,” alisema Rais Kikwete alipokuwa akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM. Alisema kazi ya uteuzi wa wajumbe hao ilikamilika tangu juzi na kinachofanyika sasa ni kuhariri majina hayo na kurekebisha mambo kadhaa. “Jumatatu (leo) tutayapitia majina haya ili tuone kama tunaweza kurekebisha. Baada ya hapo tutaweza kutangaza na inaweza kuwa siku hiyohiyo au kesho yake (Jumanne), hazitazidi siku h