Posts

Showing posts with the label Riadha

RIADHA: Ikangaa awalipua wanariadha

Image
K anali Mstaafu Juma Ikangaa Mwanariadha wa zamani, Juma Ikangaa, amesema wanariadha wengi wa Tanzania wanaponzwa na kutokuwa wakweli, huku akibainisha kuwa kutokuwapo kwa mkimbiaji wa mbio ndefu, Samson Ramadhan kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola msimu huu ni pigo kwa Taifa. Kauli ya Ikangaa imekuja siku chache baada bingwa huyo wa marathoni wa michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2006, kuondolewa kwenye kikosi cha Tanzania kitakachoshiriki michezo hiyo msimu huu. Wiki iliyopita, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid, alisema Ramadhan ambaye yuko kambini nchini China kujiandaa na michezo hiyo hataweza kushiriki kwa kuwa ni majeruhi na kama kutakuwa na uwezekano atarejea nchini kabla ya kambi hiyo kumalizika. Akizungumza na gazeti hili jana, Ikangaa alisema kuondolewa kwa Ramadhan kwenye kikosi hicho ni pigo. “Kutokuwa na mwanariadha huyo ni pigo kwa taifa, hata hivyo walifanya makosa, wasingemjumuisha kwenye wanariadha waliokwenda nje kwani awali nilisikia ni

ATHLETIC-TOURISM: 2014 Bagamoyo Historical Marathon

Image
Runners take of the good start to mark the first annual Bagamoyo Historical Marathon held in the ancient town of Bagamoyo on Sunday June 22 nd 2014. The winner of men’s Half Marathon race Ismail Juma is congratulated by the deputy Director of Sports Juliana Yassoda while surrounded by other officials. Ladies First: RT-Colonel Iddi Kipingu is awarding and congratulating ladies winners as part of promoting tourism and sports all together.  

TOC yaigomea RT: Viwango na Vigezo kuzingatiwa

Image
Mwanariadha mkongwe Tanzania Andrea Sambu Sipe (Pichani) na Musanduki Mohamed ndio pekee waliofikia viwango vinavyohitajika, kwa maelezo ya TOC hawawezi kuachwa maana viwango wanavyo. Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imelikataa ombi la Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) la kutumia mashindano ya taifa ya riadha kuteua timu itakayoshiriki kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola. Mapema jana, Katibu Msaidizi wa RT, Ombeni Zavala aliiomba TOC kuvuta subira hadi watakapomaliza mashindano ya taifa yatakayoanza Julai 12 na 13 ili kujua hatima ya kikosi chao cha Madola. “RT tunategemea kutumia mashindano ya taifa ili kupata timu itakayokwenda katika michuano ya Jumuiya ya Madola, hivyo tunaomba TOC itupe muda yatakapokwisha mashindano tutapeleka kwao kikosi kamili,” alisema Zavala. Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, alikataa ombi hilo na kusema kama RT inahitaji kuteua timu kwenye mashindano ya taifa waitumie kwenye mashindano mengine ya kimataifa na si Madola. “Hatuwezi kuw

RT safari hii mkiidhulumu taifa tutafanya mapinduzi wazi wazi

Image
Andrea Sambu Sipe Habari za kutatanisha zinasukwa za kukata jina la Andrea Sambu Sipe asiende kuiwakilishaTanzania katika mashindano ya Jumuia ya Madol a . Sambu mwezi December mwaka jana aliweza kushiriki mashindano ya DANZHOU INTERNATIONAL MARATHON nchini China ambapo alikimbia muda wa masaa 2:14:30 , muda ambao umefikia kiwango na vigezo vya kushiriki mashindano ya Commonwealth Games. Mbali na Sambu pia kuna Musa Nduki Mohamed ambaye pia amefikia muda unaotakiwa, hivyo kwa maelezo mafupi na yanayoeleweka ni kwamba ‘Hakuna mwingine zaidi ya hao wawiwili wamefikia vigezo vya kimataifa vinavyohitajika ili kushiriki mashindano hayo ambayo yatafanyika mwezi July. MASWALI MUHIMU: Kama kweli RT inataka Tanzania ipate medali lakini ikanuia kumwacha Sambu je watakuwa na maana gani? Haki ya mungu Ikulu tutagonga hodi iwapo Sambu ataachwa! Sambu ni mwanariadha pekee Tanzania aliyewahi kushinda mashindano ya dunia ya mbio za nyika; Hakuna mwingine. Angalia profile yak

RT IMEPOTEZA MWELEKEO KULIKO WAKATI MWINGINE WOWOTE

Image
Leonard Thadeo / Mkurugenzi wa michezo May 20 th , 2012 RT walifanya uchaguzi kwa MOU ambapo walisaini kwamba baada ya siku tisini viongozi watakuwa na katiba mpya ama sivyo watakuwa wamevunja mapatano, August 20 th , 2012 siku tisini zilitimia. (   Leo tarehe 20 th 2014 ni miaka miwili kamili imepita bila katiba mpya wala mafanikio yoyote katika mchezo wa riadha zaidi ya aibu kwa taifa letu. (    Inaelezwa kwamba mwaka mzima umetimia bila kikao cha kamati ya utendaji kufanyika kama ilivyo sheria, kanuni na taratibu za lazima za BMT. (    Leo hii RT imeburuzwa mahakamani (TEMEKE) kwa kudaiwa zaidi ya TSH: 20,000,000 kwa sababu ya uzembe wa viongozi wa taasisi hiyo isiyo na katiba inayotambulika. (    Mapema mwezi huu timu za kwenda kambini nje ya nchi zilichaguliwa mezani badala ya kuchaguliwa viwanjani kwa vigezo vya kushindanishwa ili walio bora wapelekwe.          Mheshimiwa waziri hata kwa macho tu hayo yanayofanywa na viongozi wa RT huyaoni,