WAKATI NIKITOA SHUKRANI KWA WOTE WALIOFANIKISHA MBIO ZA " MORINGE SOKOINE MINI MARATHON 2013" MONDULI ARUSHA.
Pamoja na shukrani zote kwa washiriki wote wa kumbu kumbu za Edward Sokoine , Gidabuday ameishukuru familia ya hayati Edward Sokoine, pia Mh. Namelok Sokoine kwa kushirikiana nae kwa karibu katika kukamilisha mchakato huo. Mwisho kabisa ametoa shukurani zake za dhati kwa ushirikiano wao wa karibu na wa dhati kutoka kwa WAZALENDO 25 BLOG na ASILI YETU TANZANIA BLOG. Bw. Wilhelm Gidabuday (kulia mwenye koti ya bluu ) akiwa na mwanariadha wa kimataifa Bw. Phaustin Baha Sulle wakisikiliza kwa makini na kuhakikisha zoezi la utoaji wa vyeti kwa washindi wa riadha unafanikiwa. Gidabuday aliyasimamia kidete kuanzisha na kuratibu mbio za "Edward Moringe Sokoine Mini Marathon 2013" ambayo imeungwa mkono na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete aliyeahidi kuwa mwakani atakuwa mgeni rasmi katika full Marathon ya kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine katika kutimiza miaka 30 toka afariki tarehe 12/4/1984 na kuzikwa kwake Monduli, Mkoani...