KAMANDA (RT) ATOKA NDUKI MOSCOW, ASEMA “TUMESHINDWA”
Rais wa chama cha riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka amerejea Tanzania wakati wanariadha wawili wakiwasili Moscow tayari kwa mashindano. Kiongozi huyo aliyetangulia siku kadhaa kabla ya wachezaji amerudi akiwa na hasira isiyo na kifani, akizilaumu vyombo vya habari kwa kile alichodai kwamba “wanahabari wanawasikiliza watembea miguu wasio na tija katika mchezo wa riadha na kuwaacha wao wenye akili zao”. Pia alinukuliwa akimwaga lawama kwa makampuni ya kitanzania kwa kukataa kudhamini chama cha riadha. “Tumeandika maandiko mengi kwa robo tatu ya makampuni nchini, lakini hamna hata kampuni moja iliyokubali” alihoji Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana. Sababu ya makampuni kukataa: Wakurugenzi wa makampuni wanajali sheria ambapo kabla ya kuidhinisha udhamini katika taasisi yoyote, ‘ cross checks na double checks’ hufanyika kwanza, ambapo kasoro zikipatikana udhamini hautolewi. Chama cha Riadha hakikufuata katiba wakati wa uc...