MAZISHI: Mwanamuziki maarufu wa Congo/Zaire Tabu Ley Rochereau afariki dunia nchini Ubelgiji
Tabu Ley Rocherea Mwanamuziki maarufu wa Kiafrika na mfalme wa muziki wa Rumba toka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Tabu Ley Rochereau amefariki dunia jana jumamosi akiwa hospitalini nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 76. Familia ya mwanamuziki huyo imethibitisha taarifa hizo na kusema mazishi yake yanatarajiwa kufanyika jijini Kinshasa baada ya mwili wake kurejeshwa. Tabu Ley ambaye jina lake halisi ni Pascal Sinyamwe Tabu, alizaliwa tarehe 13 Novemba 1937 huko Bandundu Magharibi mwa DRCongo, na umaarufu wake katika Muziki wa Rumba ulishika kasi zaidi katika miaka ya 1960. Alikuwa ni miongoni mwa Wanamuziki maarufu wa Kiafrika waliobobea katika utunzi, uimbaji na uadhishi wa nyimbo. Wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko, Mwanamuziki huyo alilazimika kuishi uhamishoni, na mwaka 1990 utawala huo ulipiga marufuku kusambazwa kwa albamu yake ya “Trop, c'east trop” au Too much is too much. Tabu Ley ni miongoni mwa Wanamuziki wa DRCongo ambao wam...