Riadha Kenya yawakana wakimbiaji
Dennis Malle (aliyesimama) ni wakala maarufu wa kuleta wakenya Tanzania kwa kupata 10% bila kujali uzalendo CHAMA cha Riadha Kenya (AK), kimesema hakina taarifa za wanariadha wake kwenda Tanzania kushiriki mashindano mbalimbali mwaka huu. Desemba 4 mwaka huu yalifanyika mashindano ya Serengeti Marathon na Desemba 8 Uhuru Marathon na kushirikisha wanariadha kadhaa kutoka Kenya ambao ilidaiwa kuwa wana barua rasmi za utambulisho kutoka AK kama inavyotakiwa kisheria. Suala la mawakala wa Tanzania kuwachukua wanariadha wa Kenya katika mashindano mbalimbali bila kufuata taratibu limekuwa likiota mizizi huku Riadha Tanzania (RT), ikishindwa kulipatia tiba. Katika mbio za Uhuru Marathon , zilizagaa habari kuwa mwanariadha Emily Lagat amefariki mara baada ya kumaliza mbio hizo, kabla ya wakala wake, Dennis Malle , kukanusha huku akibainisha kuwa ni mzima licha ya kwamba alikuwa majeruhi. Malle akizungumza kwa simu kutoka Arusha, alidai kuwa Lagat ali...