MATOKEO: Mfumo mpya ‘ahueni’ kidato cha nne
Dr Kawambwa/Waziri Elimu Kwa matokeo kidato cha nne 2013 bonyeza hapa: Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne wa 2013, huku ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 15.17. Matokeo hayo ni ya kwanza tangu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa upangaji ambao ulipanua wigo wa alama na madaraja, hivyo kutoa nafasi kubwa zaidi kwa watahiniwa kufaulu. Licha ya kuanza kutumika kwa mfumo huo, idadi ya waliofeli imeendelea kuwa kubwa kwani watahiniwa 151,187 sawa na asilimia 42.91 wamepata sifuri. Kati ya hao, wavulana ni 78,950 sawa na asilimia 41.54 na wasichana ni 72,237 sawa na asilimia 44.51. Kadhalika matokeo hayo yameendelea kushuhudia baadhi ya watahiniwa wakiandika matusi kwenye karatasi zao za majibu, huku wengine wakichora vitu vya ajabu kwenye mitihani hiyo, huku wengine wakishindwa kuandika chochote kwenye karatasi hizo. Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msond...