Posts

2016 RIO DREAMS: I am back running again after a long holiday break

Image
Yes I know this will be hard for people to believe! WHAT if I make it to Rio representing Tanzania! And WHAT if my son makes it to RIO representing United States of America in one single Olympic Games? Will it be a history or what? Hahaha I don’t know but ‘HELL YES’ Anything can happen!

HATARI: Malinzi mfukuze Nyambui RT

Image
Ni Jumatatu nyingine tena tunakutana wadau wa Uwanja wa Kuchonga, kama kawaida tukipeana changamoto za kispoti ili kuchochea ufanisi katika sekta hii muhimu katika jamii. Bila shaka mu wazima wa afya na mnaendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa kama kawaida, ila kwa wale ambao hali zao si shwari kwa namna moja ama nyingine, tunawaombea nafuu ya mapema. Kama ada, kwa manufaa ya wale ambao hatukuwa nao wiki iliyopita, tupeane dondoo japo kwa ufupi kile kilichojiri Jumatatu iliyopita. Wiki iliyopita tuliangalia sakata la usajili wa aliyekuwa kiungo wa Yanga, Frank Domayo, ambaye alinyakuliwa na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Azam FC, tukio lililowagusa mashabiki na wadau wengi wa soka hapa nchini. Lakini tulichokizungumzia, si kusajiliwa kwake Azam, bali jinsi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilivyojiingiza katika suala hilo kwa mgongo wa tukio hilo kufanyika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars, kisha kuamua kumteua Wakili Wilson Ogunde, kwa kile kilichoitwa kuc

Tupa: Sililii safari, bali jina langu kutumika

Image
Mwl. Samwel Tupa akitoa hoja KOCHA maarufu wa riadha nchini, Samwel Tupa kutoka Arusha, amefafanua kwamba anacholilalamikia Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), ni jinsi jina lake lilivyotumika kama kocha aliyeondoka na wachezaji waliokwenda New Zealand kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika Julai mwaka huu, Glasgow Scotland. Jina la kocha huyo lilitangazwa katika vyombo vya habari, kwamba ameondoka na wanariadha hao, lakini badala yake alikwenda Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, kama kocha wa wanariadha na yeye kuachwa bila taarifa. Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu akiwa jijini Arusha, Tupa alisema anacholalamika yeye ni kwanini uongozi wa RT uliamua kutumia jina lake hadi dakika za mwisho, ilhali wamemuacha. “Watu wanashindwa kuelewa, mimi silalamiki kuachwa katika hiyo safari, lakini kinachoniumiza mimi kwanini jina langu litangazwe kwamba naondoka wakati naachwa? Kwani kulikuwa na u

Tanzania ikipitisha sheria ya uraia wa nchi mbili nitaiwakilisha Olimpiki 2020

Image
“Endapo Tanzania itafanikiwa kupitisha katiba yake mpya inayosukwa hivi sasa nchini humo mimi nitafurahi kujumuika na ndugu zangu wa damu kuiwakilisha nchi hiyo katika Olimpiki 2020”   “Mimi ni mzaliwa wa Riverside, California, Marekani, kuzaliwa kwamgu hapa kulitokana na baba yangu kuja Marekani kama mwanafunzi 1993 na kwa mapenzi yake akamleta aliyekuwa rafiki wake ambaye ndiye mke wake na ndiye mama yangu hivi sasa” “Alimtafutia nafasi ya kuja kujiendeleza kimasomo na ndipo mimi nikazaliwa na wawili hao kutokana na mazingira hayo, nilipelekwa Tanzania nikiwa na miaka miwili nikakaa kwa miaka mitano na hata shule ya msingi nilianza Arusha ambapo baadaye wazazi wangu waliamua nirudi kupata elimu Marekani” “Marekani ni nchi yangu ya kuzaliwa ila Tanzania ni nchi yangu kiasili (My ancestral home), ninaipenda sana Tanzania na hata ninaposhiriki mashindano ya shule hapa California huwa wenzangu wananiitaga Tanzanian boy” CHANZO: Haya ni maneno yake Sydney Wilhelm Gi

VITUKO: Chama Cha Riadha Tanzania (RT) lawamani

Image
Mwl. Samwel Tupa KOCHA maarufu wa riadha, Samwel Tupa, ameulalamikia uongozi wa Riadha Tanzania (RT), kwa kutumia jina lake kama kocha aliyeondoka na wanariadha waliokwenda nchini New Zealand kwa maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajia kufanyika Glasgow, Scotland, Julai mwaka huu. Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu akiwa jijini Arusha, Tupa alisema hajui sababu iliyofanya uongozi huo kufanya hivyo, na kwamba mara ya mwisho aliwasiliana na Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, ambaye alimtaka wabaki ili waandae mashindano ya taifa yanayotarajiwa kufanyika Juni. “Nyambui aliponiambia hivyo, nilimwambia mimi kama kocha siwezi nikabaki wakati wanariadha wangu wanakwenda, huko watafundishwa na nani, akadai watakuwa na kocha wa China, lakini mimi sikuafiki hilo na nikajua watakuwa wamebadilisha jina la kocha anayeenda, ila cha kushangaza naona kwenye vyombo vya habari kwamba nimeenda huko,” alisema. Alisema mbali na yeye kuachwa

Gidabuday: The Tanzanian American young and up-coming athlete

Image
  Sydney Wilhelm Gidabuday with (Tanzania Uniforms) PR i Congratulations Sydney Wilhelm Gidabuday ! He competed in the 1500 Invitational and 5000 invitational heats at the Long Beach Invitational, held 4/19/14. He won the 5000m with a PR time of 14:26.30. He also broke his n the 1500m - 3:51.73, for 6th place.  Way to go Sydney! SOURCE:  Helen Moreno in California USA.

Tamasha: DAA, RT waandaa mbio za Muungano

Image
Thabit Bashir / Katibu msaidizi DAA CHAMA cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), kwa kushirikiana na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), wameandaa mashindano maalumu kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa mujibu wa Katibu Msaidizi wa DAA, Thabity Bashir, mbio HIZO zitafanyika Aprili 25 jijini Dar es Salaam na kushirikisha wachezaji kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na visiwani Zanzibar. Bashir aliitaja michezo itakayoshindaniwa kuwa ni mita 100, Relay mita 100 na 400, mitupo na mita 5,000. Alitoa wito kwa mashabiki, wapenzi wa riadha na michezo kwa ujumla, kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa, ambako kiingilio ni bure. CHANZO: Tanzania Daima