GIDAWAME GWAI MAGOMA: Nataka niwe mwanariadha wa kimataifa
Mwanariadha chipukizi (Gidawame) akikabidhiwa vifaa vya michezo na Eva Gidabuday (Mkurugunzi wa GSTF), kushoto ni Faustin Baha Sulle (mshindi wa medali ya Fedha mbio za nusu marathon za dunia Veracruz Mexico 2000) ambaye anamsimamia katika mazoezi ya mwanariadha huyo Gidawame alizaliwa tarehe 28/12/ 2000 a kiwa mtoto pekee kwa mama yake ambaye alifariki akiwa bado mdogo sana kiasi kwamba hakumbuki sura yake. Baada ya mama yake kufariki akalelewa na mama wa kambo kwa sababu Baba yake alikuwa na wake tisa ikiwa ni pamoja na mama yake aliyefariki. “Nilipitia maisha ya mateso sana nikiwa mikononi mwa mama zangu wa Kambo, nilinyimwa haki zangu za msingi, nililazimika kuchunga ng'ombe; hata ilipofika wakati wa kuanza shule nikanyimwa kwenda shule wakati wenzangu wengine wakisoma” Kitendo cha kunyimwa kusoma kilimumiza sana, ikafika wakati akiwa machungani anawasogeza ng’ombe karibu na shule ili aweze kuwasikia wenzake wakisoma naye apate kujifunza. Wazazi walipopata taarifa walim