Posts

Showing posts with the label Matukio

Taswira ya Dodoma Hapa Kazi Tu Half Marathon

Image
Mheshimiwa Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza mbio za kilomita 2.5 Waheshimiwa mawaziri na wabunge wakiendelea na mazoezi yao siku ya mbio Filbert Bayi akiwa katikati ya waandishi na wadau waliokuwa wakimhoji siku ya mbio

Kuelekea maandalizi ya Mbio za Dodoma

Image
Mwingereza & Gidabuday Kocha wa riadha Anthony Mwingereza akiwa na Wilhelm Gidabuday Dodoma mwishoni mwa wiki kwa maandalizi ya mbio za Dodoma Hapa Kazi Tu Half Marathon. Mbio hizo zimeandaliwa na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kwa madhumuni ya kuendeleza mchezo wa riadha nchini. Pia mbio hizo zimeandaliwa kama mchakamchaka wa kupasha misuli kuelekea mashindano ya Olimpiki ya Rio De Janeiro nchini Brazil mwezi August mwaka huu.

Preps for Rio Olympic Games

Image
Coach Francis John (Lft) National Athletics Coach for Rio De Janeiro Games Mr Francis John says his boys are ready for medals. Tanzania has so far produced only two marathoners who have qualification standard for Rio Games. The two athletes who have their tickets ready for the games are Alfonce Felix and Said Makula, Felix qualified last year in Australia while Makula qualified at Casablanca Marathon. Said Makula, Gidabuday & Alfonce Felix

Canadian Government abused human rights when acupied Barbaig land

Image
"I read this old archive report about the hardship brought to Barbaig community by Canadian Government, Canada is regarded as one of world's leading countries to hate human rights abuses! Barbaig community should reopen the case in the international court for retribution|" A disastrous project funded by the Canadian Government is destituting an African people By George Monbiot. Published in the Guardian 23rd November 1994. To the Barabaig people of Tanzania, home is where the dead lie. When a man dies, a mound is built for his spirit to inhabit. A holy tree is planted beside it, under which his descendants pray for his blessing and protection. To these nomads the mounds are the fixed points around which their migrations range, the spiritual focus of their lives. A land without spirits is a no man’s land. Today the last of the spirit mounds of the Basotu Plains, the Barabaig’s critical wet season grazing lands, are being ploughed up by a development pr

Rais Dr John Magufuli atangaza baraza jipya la mawaziri

Image
Rais Dr John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hivi punde ametangaza baraza lake la mawaziri, amesema wizara nyingi wameunganisha na atakuwa na wizara 18, na watakuwa na mawaziri 19 tu, na baadhi ya wizara zitakuwa na manaibu waziri huku zingine hazitakuwa na manaibu waziri. Magufuli: Baraza nitakalolichagua halitakuwa na semina elekezi, kama ni semina watajipa huko huko ndani, wenyewe. Baadhi ya Wizara na Mawaziri wake;   Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora – Simbachawene na Angela Kairuki. Wizara ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ina mawaziri wawili ambao ni Mh. Simbachawene na Kairuki Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Waziri wake ni Jenesta Mhagama Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa – Augustino Mahiga, Naibu Waziri – Dk. Suzan Kolimba Wizara ya Ardhi – William Lukuvi Wizara ya Elimu Waziri bado hajapatikana, Naibu Stella Manyanya Waziri wa Afya Jinsia na Watoto: Ummy Mwalimu, Naibu

Gidabuday amaliza # 6 mbio za nyika Marekani

Image
Sydney Wilhelm Gidabuday Sydney Wilhelm Gidabuday alimaliza mbio za nyika za kilomita 10 kwa kutumia dakika 29 sekunde 39 jimbo la Missouri nchini Marekani. Alishika nafasi ya sita kati ya wanariadha 246 ambao walifuzu kuwakilisha vyuo vyao katika mashindano ya fainali za National Collegiate Athletics Associations (NCAA) Katika mashindano hayo Gidabuday alianguka ikiwa amebakiza kilomita tatu, alipitwa na umati mkubwa, alipoinuka alianza tena kufukuza upepo na kuwakuta wengi waliompita akafanikiwa kuishia namba sita. Mshindi wa mbio hizo Alfred Chelanga alikimbia dakika 29 sekunde 24. Gidabuday aliiwezesha Adam State University kushika nafasi ya pili yeye akiwa mkimbiaji nambari moja wa chuo chake. “I fell half way through, but was able to finish 6 th with the time of (29:39), it socks to be beaten by those whom I know I could beat” Gidabuday aliyasema hayo akihojiwa na Espn-Tv.

Mafisadi Hananag wauza Viwanja, Vyanzo vya Maji

Image
Mt Hanang / Mlima wa tatu Tanzania Wilaya ya Hanang ina bahati ya kuwa na mlima wa tatu Tanzania (Mt Hanang 3,417m) baada ya (Mt Kilimanjaro 5,895m ) na (Mt Meru 4,565m) , milima yote mitatu ikiwa kanda ya kaskazini mwa Tanzania. Mwenyezi mungu ametujalia utajiri wa misitu, wanyama na maji, lakini binadamu wamekuwa mafisadi na wababe, kufikia hatua ya kubadili matumizi ya utajiri huu kwa kutumia mabavu, pesa na rushwa. Ni miaka mingi hivi sasa tangu serikali ilipoamuru wavamizi wa Bonde la mto Endamanang kuondoka, hata ilani iliwekwa na serikali; lakini kwa sababu ya ulafi wa baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi wakishirikiana na viongozi wakuu wa wilaya ya Hanang wasio waaminifu ilani iliharibiwa, hadi leo hii Bonde la Endamanang bado linalimwa na watu kumi tu. Hawa hapa wanaolima Bonde la mto Endamanang lililopo Nangwa - Hanang kwa kulindwa na polisi wa Hanang ; (1)Nino Yahhi, (2)Sikukuu Axwesso, (3)Damasi Yatosh, (4)Disdery Yatosh,  (5)Izraeli

Vigogo TRA walikutwa na mamilioni majumbani mwao

Image
Fedha taslimu iliyokutwa kwa vigogo Siku  chache baada ya kigogo mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kubainika kumiliki nyumba 73, wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo wamekutwa na mamilioni ya shilingi waliyoficha majumbani mwao. Taarifa kutoka ndani ya TRA zinapasha kuwa tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awasimamishe kazi maofisa kadhaa wa mamlaka hiyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kitengo cha uchunguzi cha mamlaka hiyo, hivi sasa wapo kwenye msako wa kubaini ukwasi wa wafanyakazi wake. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, juzi maofisa wa kitengo cha uchunguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, walifika katika eneo la Tegeta Salasala wilayani Kinondoni na kuvamia nyumba mbili za wafanyakazi wa mamlaka hiyo. Katika nyumba hizo, wafanyakazi hao kila mmoja alikutwa na kiasi kikubwa cha fedha ndani kuliko kiwango cha mshahara anaolipwa. “Walivamiwa wafanyakazi wawili (majina yanahifadhiwa), ambapo katika kila nyumba zilikutwa fedha nyi

Ikulu yakanusha kutoa ratiba

Image

Baraza la Mawaziri Kenya labadilishwa

Image
Rais Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri na kuwaacha wote ambao wizara zao zilikumbwa na tuhuma za ufisadi. Rais Uhuru Kenyatta amechukua hatua hiyo siku moja tu baada ya kutangaza ufisadi kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa. Rais ameahidi kufanya mabadiliko zaidi katika afisi yake hivi karibuni. Katika hotuba ilioonyeshwa kwa njia ya Televisheni, Rais Kenyatta ameongeza idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara mbalimbali katika kile alichosema ni kusaidia mawaziri kutekeleza majukumu yao bora zaidi. Idara hizo zimeongezwa kutoka 26 hadi 41. Rais Kenyatta amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri baada ya mawaziri sita kulazimika kujiondoa kutokana na wizara walizosimamia kuhusishwa na ufisadi huku wawili kati yao wakikabiliwa na kesi mahakamani. Ni mabadiliko yaliyotarajiwa hasa baada ya hatua ya aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kujihuzulu mwishoni mwa jum

Wanariadha walioing’arisha Tanzania Mbio za Nyika warejea

Image
Kocha Francis John, Joseph Panga, Bazil John, Suleiman Nyambui, Alphonce Felix, Ismail Juma wakiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere. Wanariadha watano wa timu ya taifa ya riadha wamewasili jana wakitoka kuiwakilisha   nchi katika mashindano ya dunia ya mbio za nyika yaliyofanyika mjini Guiyang, China mwanzoni mwa juma hili. Tanzania ilishika nafasi ya sita katika nchi 51 zilizopeleka wanariadha kwenye mashindano hayo huku Ismail Juma akitua nafasi ya tisa kati ya wanariadha 111 waliokimbia kilometa 12. Timu hiyo iliwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 10:55 jioni kwa Shirika la Ndege la Emirates wakiongozana na Kocha wao Francis John na kupokewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini (RT) Suleiman Nyambui. Pia mwanariadha Bazil John alisema kuwa Tanzania isitegemee medali kama haiwekezi katika maandalizi kwani wamejifunza mengi walipoenda kushiriki mbio hizo. Kocha Francis John alisema hata sasa wanariadha wamejitahidi sana kutokan