JUMA IKANGAA: “The will to win is nothing without the will to prepare”
Juma Ikangaa Juma Ikangaa ni kati ya wanariadha wachache sana duniani waliodhaminiwa na kampuni moja ya viatu kuanzia mwanzo wa harakati zake za riadha hadi kustaafu kwake bila kuhama hama kimasilahi. Nchini Japan Juma Ikangaa anafahamika kuliko hata viongozi wakubwa wa nchi kutokana na uaminifu mkubwa aliouwekeza wakati akishiriki riadha chini ya udhamini wa kampuni ya vifaa vya michezo ya ASICS ya Japan . Mwaka 1984 katika Olimpiki ya Los Angeles California , kwa heshima ya Juma Ikangaa, kampuni ya vifaa vya ASICS ya Japan iliipatia timu ya Tanzania vifaa vyote kwa timu nzima ya Tanzania, kati ya vifaa vingi vilivyotolewa na kampuni hiyo ni pamoja na (track suits 1,000) ambazo kwa sasa Riadha Tanzania haiwezi kupata kutokana na sura mbaya iliyojengeka baada ya makampuni mawili ya PUMA na LINING kuhujumiwa na viongozi wa RT na TOC ambao baadhi yao hadi sasa wapo katika uongozi wa vyama hivyo. 'Ndiyo maana hata leo huko Morogoro wanariadha chipukizi wanakimbia peku hali mak...