Posts

TUZO ZA KILI 2014 ZIMEZINDULIWA LEO N AKUFANYIWA MABADILIKO

Image
Ni time ya kufahamu kuhusu tuzo ambazo hutolewa kwa Wanamuziki/Wasanii mbalimbali wa Tanzania zikiwa zimeanzishwa mwaka 1999 ambapo za mwaka huu 2014 zimezinduliwa leo February 17.     George Kavi she kutoka TBL ambao ndio Wadhamini wa tuzo hizi amesema ‘Maboresho makubwa ambayo tumefanya mwaka huu ni tofauti na mara zote ambazo tumekua tukihusisha Watanzania dakika za kupiga kura tu hivyo wanakosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye category gani, mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani’ ‘Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura z...

Simba, Mbeya City zavunja rekodi

Image
PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), kati ya wenyeji Mbeya City na Wekundu wa Msimbazi, Simba lililopigwa juzi Uwanja wa Sokoine, limevunja rekodi ya mapato baada ya kuingiza sh milioni 105. Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, na kujaza melfu ya mashabiki, tiketi 21,000 ziliuzwa na baada ya makato, kila timu iliondoka na sh 25,316,630.58. Kwa mujibu wa msimamizi wa Kituo cha Mbeya, Lwitiko Mwamundela, mgawanyo mwingine ni VAT sh 16,016,949.15, gharama za uwanja sh 12,872,702.57, gharama za mchezo sh 7,723,621.52 na Bodi ya Ligi sh 7,723,621.52. Mgawo mwingine ni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sh 3,861,810.75 na Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA) sh 3,0003,630.58. Msimamizi huyo aliongeza kuwa mapato hayo yamevunja rekodi ya mchezo wa mazunguko wa kwanza kati ya Mbeya City na Yanga, ambao uliingiza sh milioni 100 zilizotokana na mauzo ya tiketi 20,000. Hata hivyo, licha ya mchezo huo kuingiza kiasi hicho cha fedha, changamoto ilikuwa ni uch...

Kili Marathon yatangaza njia mpya

Image
WAANDAAJI wa Kilimanjaro Marathon wametangaza njia mpya zitakazotumika mwaka huu, ikiwa ni hatua nyingine muhimu katika mafanikio ya mbio hizo ambazo zinaingia mwaka wa 12 tangu kuanzishwa. Njia hizo mpya zimelenga kuboresha mwendo wa washiriki barabarani na kuwafanya wafurahie zaidi mbio hizo zilizopangwa kufanyika Machi 2 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Akitangaza njia hizo mpya jana, John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo, alisema wameanzisha njia mpya ili kuzuia msongamano wa watu wakati wa mbio kutokana na kuongezeka idadi ya washiriki kila mwaka. Addson alisema washiriki wa mbio ndefu za marathon km 42, nusu marathon km 21, mbio za walemavu na mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run, sasa hawatapishana tena barabarani, bali kila njia itatiririka katika muelekeo mmoja. “Pia kutokana na mabadiliko haya, washiriki watakuwa wameepuka kilomita 3 za mwinuko mkali kuelekea Chuo cha Mweka ambapo awali ndipo palikuwa mahali pa kugeu...

Nyambui: Tujitoe Madola

Image
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui, ameitaka Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kuifuta Tanzania kushiriki mashindano ya kimataifa hadi itakapokuwa imefanya maandalizi ya kutosha. Kauli hiyo ya Nyambui imekuja wakati akitoa maoni yake juu ya ushiriki wa Tanzania katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Glasgow, Scotland baadae mwaka huu. Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Nyambui alisema kama nchi inataka kupata mafanikio katika mashindano hayo inapaswa kujipanga kuanzia ngazi ya vijana kwani ndiyo msingi wa mafanikio ya michezo yote. Alisema kinachoiponza Tanzania ni maandalizi. “Mbona zamani walifanya vizuri kwa nini sasa hivi washindwe,” alisena na kuongeza kwamba Tanzania ya sasa si kama ile ya zamani wakati wao wanaiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali. “Siku zote shule ndiyo zinaibua vipaji, kama zikiwa nzuri hata timu za taifa zitakuwa nzuri pia,” alisema Nyambui ambaye pia ni mjumbe ...

Rogart John, Phaustin Baha na Gidabuday wakiwaza namna ya kuhamasisha riadha

Image
Rogarth, Faustin & Gidabuday/Photo by Gadiola Siku ya kwanza kuwaza mbinu za kupeleka wazo la Sokoine Mini Marathon kwa wahusika tulikuwa watatu na ilikuwa kazi sana kutokana na upinzani kutoka kwa wanaojiita ‘Viongozi wa RT/TOC’ Kila mtanzania anayo jukumu la kubuni mbinu mbadala kusaka vipaji, kukuza vipaji na kuhamasisha taifa kuwa mstari wa mbele kuchangia gharama za timu zetu za vijana hatimaye kufuzu timu za taifa. Lakini kwa bahati mbaya Ubinafsi, Wivu na Ukabila umetawala katika chama cha riadha na kamati ya Olimpiki. Kwa mawazo yao “Bila Filbert Bayi na Suleiman Nyambui watanzania hawawezi lolote”. Wamefanikiwa kuwaaminisha wengi kwa kuwapotosha ili wao watukuzwe. Hadi leo ni wazi kwamba Sheria # 12 za BMT zilizotungwa na Bunge 1967 zilivunjwa makusudi ili kuwazuia watu wawili tu wasiingie katika uongozi wa RT! Je Bayi, Nyambui na Mtaka wana nguvu kumshinda Jakaya Kikwete anayesisitiza sheria kufuatwa?. Bila shaka tutakuwa na JK siku zija...

President Kikwete spoke to CNN’s Christiane Amanpour

Image
“At independence Tanzania had 350,000 elephants… in 1987 there were only 55,000 elephants left.” That’s the dire message from the president of Tanzania, who spoke to CNN’s Christiane Amanpour about his country’s battle against wildlife poaching. President Jakaya Kikwete joined Amanpour in London, where heads of state are meeting to find a solution to end poaching before it’s too late. “This is madness now, it is just impossible… it’s a serious matter.” Incidents of poaching are on the rise fueled by a growing demand for ivory and rhino horn in Asia. There are also concerns that poaching is helping to fund violent groups in the region. When it comes to destroying ivory stockpiles, as countries like the United States and China have done in the past, President Kikwete says his country is considering doing the same thing to show it is an unacceptable trade. “We have about 112 tonnes of ivory… we used to have the idea of asking permission to sell, but we don’t think, thes...