Yaliyojiri Sokoine Mini Marathon 2014
MWISHONI mwa wiki, Aprili 12 mwaka huu, macho na masikio ya Watanzania wengi yalielekea katika Kijiji cha Monduli Juu, kilichopo Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha, kufuatilia kumbukumbu za miaka 30 tangu kufariki kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine. Maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, yaliadhimishwa kwa matukio mengi ya kukumbukwa, lakini moja ya matukio yaliyotokea katika kumbukumbu hizo, ni msimu wa pili wa mbio za Sokoine Mini Marathon mwaka 2014. Mbio hizo zilianza majira ya saa mbili asubuhi, ambapo pamoja na kuwepo kwa ushindani mkubwa, kulikuwa na matukio mengi yasiyo ya kawaida, likiwemo la wanariadha kulazimika kupisha magari. WANARIADHA WANASA KWENYE TOPE Zikiwa zimesalia takribani kilomita mbili mbio za kilomita 10 zimalizike, wanariadha walijikuta wakibadilishana baada ya njia kujaa matope huku kukiwa na mgari mengi yaliyokwama barabarani. Tukio hilo lili...