TOC yaigomea RT: Viwango na Vigezo kuzingatiwa
Mwanariadha mkongwe Tanzania Andrea Sambu Sipe (Pichani) na Musanduki Mohamed ndio pekee waliofikia viwango vinavyohitajika, kwa maelezo ya TOC hawawezi kuachwa maana viwango wanavyo. Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imelikataa ombi la Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) la kutumia mashindano ya taifa ya riadha kuteua timu itakayoshiriki kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola. Mapema jana, Katibu Msaidizi wa RT, Ombeni Zavala aliiomba TOC kuvuta subira hadi watakapomaliza mashindano ya taifa yatakayoanza Julai 12 na 13 ili kujua hatima ya kikosi chao cha Madola. “RT tunategemea kutumia mashindano ya taifa ili kupata timu itakayokwenda katika michuano ya Jumuiya ya Madola, hivyo tunaomba TOC itupe muda yatakapokwisha mashindano tutapeleka kwao kikosi kamili,” alisema Zavala. Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, alikataa ombi hilo na kusema kama RT inahitaji kuteua timu kwenye mashindano ya taifa waitumie kwenye mashindano mengine ya kimataifa na si Madola. “Hatuwezi kuw...