Okwi arejea Simba
Emmanuel Okwi /Mchezaji maarufu wa soka HATIMAYE mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, jana amesaini kuichezea klabu yake ya zamani ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili. Habari zilizopatikana jana jioni, zilisema nyota huyo ambaye hatima yake ndani ya klabu ya Yanga ilikuwa gumzo kubwa, jana alitarajiwa kusaini mkakaba huo kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi kwa kipindi kingine. Kurejea kwa Okwi Msimbazi, kunamweka katika wakati mgumu mchezaji Benard Musoti, nyota wa kimataifa wa Kenya, kwani sasa ni yeye sasa anayechungulia dirisha la kutokea, ama Pierre Kwizera. Okwi kutua Simba, ni kama kurejea nyumbani kwani ndio klabu aliyojiunga nayo kwa mara ya kwanza nchini akitokea Uganda na kung’ara nayo, kabla ya kuihama na kujiunga Etoile du Sahel ya Tunisia na kisha Yanga. Sheria za usajili za Ligi Kuu Tanzania Bara zinataka klabu kuwa na nyota wa kigeni wasiozidi watano na mbali ya Okwi, nyota wengine wa kimataifa katika kikosi cha Simba ni, Raphael Kiongera, Joseph O...